Ajira 17,412 kwa kada za Elimu na Afya zatangazwa. Wananchi wenye sifa wahimizwa kuomba nafasi

Ajira 17,412 kwa kada za Elimu na Afya zatangazwa. Wananchi wenye sifa wahimizwa kuomba nafasi

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa, amewataka Watanzania wenye sifa waombe nafasi za kazi kuanzia leo, baada ya serikali kutangaza nafasi za ajira 17,412, kwa kada ya elimu na afya.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 20, 2022, Bungeni Dodoma, wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Nimshukuru Rais Samia kwa kutoa idhini ya ajira za watumishi wa afya na elimu 17,412, ambapo nafasi 9,800 ni za walimu na 7,612 ni kada za afya ambao wataajiriwa mwaka huu wa fedha 2021/22, nitoe taarifa rasmi kwamba Watanzania wenye sifa wanaelekezwa kuomba kuanzia leo, maombi ya ajira hizi ni bure," amesema Waziri Bashungwa.
 
Hawajafungua,Waziri ananena tu,kuwahadaa watu wasiokua na uelewa.Wafungue ili kwa ambao koneksheni hakuna,waombe,waangalie Bahati zao.
 
Siasa bhana,hapo wazazi wakimsikia Waziri alivyosema,wanakua hawawaelewi watoto wao pale wakijibiwa BADO hawajafungua system.Magu ana madhaifu yake,ila alikua hapendi ujingaujinga.
 
Siasa bhana,hapo wazazi wakimsikia Waziri alivyosema,wanakua hawawaelewi watoto wao pale wakijibiwa BADO hawajafungua system.Magu ana madhaifu yake,ila alikua hapendi ujingaujinga.
Wazaz wanakuona hufatilii mambo ya muhimu
 
Back
Top Bottom