Ajira hii ni zaidi ya faida yako?

Ajira hii ni zaidi ya faida yako?

Joined
May 18, 2023
Posts
27
Reaction score
38
Hii Ajira sasa imekuwa tegemezi sana kwa vijana na wengine wenye imani tofauti wakiamini ipo siku watakusanya kiasi cha pesa nyingi kupitia hii Ajira .

Hivi karibuni kwa asilimia kubwa zaidi za vijana mwanga wao ndo hii Ajira ambayo imekuwa ikileta waumimini wapya kila kukicha na kuwafanya kuwa waumini wa kugalagala bila kuchoka au kujari ni kiasi gani cha mtaji kinacho watoka . Kwasababu ya ule uwezekano wa kuipata faida hiyo ya ghafla.

Imekuwa ni tegemezi mno la kimya kimya kwa kila muumini kuwa wenda nitajirimbikizia pesa kupitia hii Ajira mkombozi. Lakini kwa kuendelea na bila kukoma mwisho tumaini linapotea lakini imani ya tamaa bado inafanya kazi kuhimiza kuendelea kuamini ipo siku Ndiyo.

Hii Ajiri kuna baadhi ya watu imewakumbuka na kuwafanya vile walivyo Dhania awali ila kwa wengi ni bado hii Ajira aitimizi Ahadi sawa na vile kijana anavyo taka

●●○》》 Ushauri wako kuhusu hii Ajira ya "BETTING " Kwa vijana kama mwa jamii forum unaye zingatia faida za kiuchumi zaidi utazungumza nini kuhusu ukweli huu wa hii Ajira ni Mbinu gani itumike kuakikisha hii Ajira ina mpa kijana faida .

NB; Naomba tujikite tu kwenye faida na namna ya kuutumia vizuri hii Ajira au huu mchezo wa betting na siyo Harasa maana bado vijana awasikii tukiwapa madhara. Tuwatie moyo kwa kuwaelekeza kwa faida namna ya kunufaika na Mfumo. Ili wasi lie kila siku.

20240407_204258.jpg
 
Hakuna pesa ya bure ya kupata kisa umebashiri matokeo ya kitu fulani,hicho kitu uwe umebashiri au haukubashiri kama kilikuwa kipate matokeo mazuri au mabaya kutabiri kwako hakungekisaidia au hakungekipunguzia chochote.

Hela inatafutwa kwa jasho,kwa kujibidiisha,kujenga tabaka la uaminifu kwa jamii na taifa,kutumia skills mtu alizopewa(kila mtu ana kitu cha ziada ndani mwake kinahitaji msukumo ili kionekane) kama ni biashara au ajira serikalini hauwezi kuwa bora ikiwa utakaa na kufanya utendaji mbovu huku ukiiaminisha akili yako kwamba kuna hela za bure utapata ukibashiri kitu fulani.

Mchezo wa kubet ni hasara kwa taifa nguvu ya taifa ile ya kuamka asubuhi na kukuna kichwa siku iende vipi haipo,vijana wengi leo wanajivunia mambo mbalimbali waliyoyafanya wazee wao hayo hayakufanyika wakiwa wamejifungia ndani au vijiweni wakipeana mbinu za kupata hela bure walitoka kwenda kutafuta kwa uchu na wakafanikiwa.
 
Hakuna pesa ya bure ya kupata kisa umebashiri matokeo ya kitu fulani,hicho kitu uwe umebashiri au haukubashiri kama kilikuwa kipate matokeo mazuri au mabaya kutabiri kwako hakungekisaidia au hakungekipunguzia chochote.

Hela inatafutwa kwa jasho,kwa kujibidiisha,kujenga tabaka la uaminifu kwa jamii na taifa,kutumia skills mtu alizopewa(kila mtu ana kitu cha ziada ndani mwake kinahitaji msukumo ili kionekane) kama ni biashara au ajira serikalini hauwezi kuwa bora ikiwa utakaa na kufanya utendaji mbovu huku ukiiaminisha akili yako kwamba kuna hela za bure utapata ukibashiri kitu fulani.
Mimi siungi mkono betting lakini kuna mtu ninayemfahamu vizuri alipiga million 100 plus.

Akili zake hakujiongeza kama ule ni mtaji zile pesa zote amemaliza na life yake Kwa sasa ni tia maji tia maji.

Kwa kifupi kamari haifai hata ipewe Jina gani.
 
Serikali inacho angalia ni yenyewe itapata faida kiasi gani kutoka kwa huyo muwekezaji? Ukitimiza Vigezo na Masharti unapewa ruhusa.

Tatizo lipo kwa vijana kuingia kwenye Mchezo wa Ajira bila kuwa na Akili ya Ufahamu toshelevu namna ya kupata Faida. Hivyo, kuishia kupata hasara na hasara yao ndiyo faida kwa wengine wachache na ndiyo malipo ya kodi kwa Serikali huku Mwekezaji akiendelea kupata faida.

Wenye Akili na Ufahamu kilasiku wanajichukulia Fedha kupitia mchezo huohuo.

Tanzania yetu TATIZO NI ELIMU.

Nionyeshe Mtoto wa Kiongozi anayesoma Kayumba, Nami nikuonyeshe ukweli halisi namna ya kupata fedha halali kilasiku kupitia Betting.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom