SoC01 Ajira kupitia kukusanya vifaa vibovu vya wateja na kuvipeleka kwenye matengenezo

SoC01 Ajira kupitia kukusanya vifaa vibovu vya wateja na kuvipeleka kwenye matengenezo

Stories of Change - 2021 Competition

Tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Posts
63,730
Reaction score
111,542
Kuna eneo linaweza kutoa ajira, japo litahitaji mtaji mkubwa kidogo. Wangalau 50m itawezesha kuendesha huduma hii. Inafahamika kuna watu wengi wanaobanwa na kazi siku nzima kiasi kukosa muda, na wengine hawana ufahamu wa kutosha sehemu ya kuweza kupata huduma mbalimbali.

Makundi tajwa hapo yote huhitaji huduma mbali mbali hasa ya matengenezo ya vifaa vyao. Mfano wa vifaa hivyo ni computers, Television, Redio, Simu, Majiko ya umeme, Microwave, Majokofu (fridge), kupelekewe nguo Dry cleaners nk. Kutokana na watu kubanwa na shughuli, ama kutokujua sehemu sahihi ya kupata mafundi wa vifaa hivyo, iwapo atatokea mtu au kampuni ya kukusanya vifaa hivi na kuvipeleka sehemu ya matengenezo, kisha vikishatengamaa kuvirejesha kwa wahasika tayari kwa malipo itakuwa na tija sana. Inawezekana kabisa kutengeneza application ambayo wahitaji wataripoti mahali walipo, ili kifaa chake kifanyiwe matengenezo, aidha itakuwa ni kwa kufuatwa alipo iwe ofisini kwake, ama nyumbani.

Hapa uhitaji wa gari hasa aina ya pickup, pikipiki ama bajaji ni lazima kampuni iwe nazo, ndio maana nimekadiria wangalau 50m itatosha kwa kuanzia. Mteja anaweza kutoa taarifa ya ubovu wa kifaa chake kupitia hiyo app kama ilivyo ya Uber, kisha atapewa gharama ya kuchukua kifaa chake, na gharama kifaa kitaporejeshwa. Baada ya kifaa kupelekwa kwa mafundi wahusika, mteja atapewa gharama za matengenezo, na akiafiki atatoa hela ya matengenezo. Jukumu la kufuatilia kifaa kama kimekamilika itakuwa na mtu huyu ama hiyo kampuni itakayoamua kufanya kazi hiyo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom