A
Anonymous
Guest
Mkeka wa ajira ulitoka Januari 19 mwaka 2026. Hadi kufikia februari 10 mwaka huu waajiriwa wapya wote walikuwa wameripoti kazini.
Halmashauri ya Ushetu mpaka sasa haijalipa posho ya kujikimu kwa kada zote na kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu hilo.
Jibu la awali lilikuwa kwamba pesa haijatoka TAMISEMI, lakini baada ya kuwapa rejea za halmashauri nyingine ambazo tayari wamelipa ikabidi ziundwe mbinu za kutumyamazisha.
1. Kada ya afya waliambiwa kuandika barua na waliandika ila hatujaona majibu toka februari 10 mwaka huu.
2. Kada ya ualimu tuliambiwa tuwape wakuu wa shule gharama ya nauli tu na ilikuwa ni meseji kwa wakuu wa shule iliyosisitiza kuhakikisha walimu wapya hatujui kinachoendelea halmashauri ili tusipige simu kuuliza pesa hizo.
3. Kada ya kilimo na mifugo hawajawahi ambiwa lolote.
Viongozi wa idara wakiulizwa wanadai wajibu wao kwa ngazi ya halmashauri wametimiza, imebaki mamlaka ya kulipa ilipe.
Sasa tunajiuliza, TAMISEMI ina makundi?
Hatujui lini tutalipwa na vitisho ni vingi. Mkurugenzi hafikiki kiukweli, wazoefu wanakwambia yule sio wa kumwingia kirahisi.