KERO Ajira Mpya Geita hatujalipwa fedha za kujikimu tangu Machi 2025

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mtumishi Ajira mpya 2025, tumeripoti kazini tangu Machi 2025 Mkoa wa Geita ila cha ajabu mpaka sasa tumemaliza takribani miezi 10 hadi 11 hatujapewa hela za kujikimu.

Imekuwa kama mpira wa kona, hatuelewi kinachoendelea, kila kiongozi ukiuliza anasema hajui au hana jibu na kutuambia kuuliza katika ofisi fulani ambapo napo ukienda hawana majibu.

Tukimuuliza Mkurugenzi naye anasema ameshatuma kwa RAS, napo hakuna kinachoeleweka, sasa tupo kama gizani hatujui A wala Z, tunaomba ujumbe huu ufike Serikali Kuu kwa Viongozi wa juu watambue kuwa kila siku Watumishi tunalilia kupata haki yetu, hii itaendelea hadi lini?
 
Wanakuambia, "Nyinyi mlikuwa mtaani mnateseka na maisha, hamna hata hela ya kula, leo hii serikali imewaonea huruma imewaajiri, mnaanza kuona eti inawatesa kwa kutowapa hiyo hela ya kujikimu"
 
Mimi ni Mtumishi Ajira mpya 2025, tumeripoti kazini tangu Machi 2025 Mkoa wa Geita ila cha ajabu mpaka sasa tumemaliza takribani miezi 10 hadi 11 hatujapewa hela za kujikimu.

Imekuwa kama mpira wa kona, hatuelewi kinachoendelea, kila kiongozi ukiuliza anasema hajui au hana jibu na kutuambia kuuliza katika ofisi fulani ambapo napo ukienda hawana majibu.

Tukimuuliza Mkurugenzi naye anasema ameshatuma kwa RAS, napo hakuna kinachoeleweka, sasa tupo kama gizani hatujui A wala Z, tunaomba ujumbe huu ufike Serikali Kuu kwa Viongozi wa juu watambue kuwa kila siku Watumishi tunalilia kupata haki yetu, hii itaendelea hadi lini?
 
Tengenezeni groups whatsapp, telegram, tengenezeni pages Facebook, Instagram nk

Muweke malalamiko yenu katika mpangilio mzuri walau hata kwa kanda fulani then kwa umoja wenu mkadai haki yenu.
 
Back
Top Bottom