Wanaukumbi.
Serikali tuliiamini na tukavumilia mateso ya mtaani tukijipa matumaini makubwa kuwa mnaijenga nchi baadae mambo yatakuwa mazuri, kumbe fedha zinatumiwa hovyo, mlikuwa na uwezo wa kuajiri kila mwaka na kuongeza mishahara ila mliamua kubana ili hizo hela za umma na kufanya ufisadi kama ripoti ya CAG, inavyosema.
CAG anaonesha namna mabeberu wetu walivyokuwa wanaitafuna hii nchi, huku wamejificha kwenye kimvuli cha uzalendo.
Ripoti hii ya CAG imetuonyesha kuwa:
- Tunahitaji taasisi imara na siyo fikra za mtu mmoja anayejidai imara
- Tunahitaji wanasiasa visionary wanaojali maslahi ya muda mrefu ya Watanzania na vyama imara vya siasa.