A
Anonymous
Guest
Kwanza, napenda kuwashukuru kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwapa wananchi nafasi ya kutoa maoni, changamoto na kero zao kupitia jukwaa hili.
Ninaomba kupaza sauti kuhusu suala la malipo ya hela ya kujikimu kwa baadhi yetu tuliokuwa tumeajiriwa katika Hospitali ya KCMC kwa mkataba na baadaye tukahamishiwa Serikalini kuanzia tarehe 1 Aprili 2025.
Hadi sasa, mwaka 2026, bado hatujapokea hela yetu ya kujikimu. Kinachotusikitisha zaidi ni kwamba kuna watumishi walioajiriwa kabla yetu ambao walipata stahiki hiyo, lakini sisi kila tunapofuatilia tunaambiwa hakuna fedha.
Tunaomba mamlaka husika zilitazame upya suala hili na kutupatia stahiki zetu kwa wakati, kwani ni haki yetu kama watumishi. Pia tunaomba JamiiForums mtusaidie kulifikisha suala hili kwa wahusika ili lipatiwe ufumbuzi wa haki na wa haraka.
Tunawashukuru kwa kuendelea kuwa sauti ya wananchi.