KERO Ajira Mpya Nzega DC hatujalipwa pesa ya kujikimu tangu Feb 2025

KERO Ajira Mpya Nzega DC hatujalipwa pesa ya kujikimu tangu Feb 2025

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sisi watumishi wa ajira mpya katika halmashauri ya Wilaya ya Nzega yaani Nzega DC hatujalipwa pesa yetu ya kujikimu tangu mwezi Februari 2025 hadi leo
Hakika hii ni changamoto sana kwa Nzega DC, viongozi wa juu waokoe jahazi.
 
Sisi ajira mpya wa wilaya ya Nzega DC tumepewa pesa ya kujikimu tarehe 30/05/2026 kiasi cha Tsh 650,000/= badala ya 150000×7 = 1,050,000/= ukijumlisha na nauli uliyotumia wakati wa kuja kuripoti kazini.

Mbaya zaidi viongozi wetu hawasemi chochote juu ya hili, sisi tunashindwa kuelewa tupo njia panda.

Tunaomba tulipwe kiasi tunachostahili kulipwa kulingana na Miongozo iliyowekwa na serikali.
 
Mimi ni mtumishi wa AJIRA MPYA 2026 katika halmashauri ya wilaya ya Nzega -Tabora, idara ya elimu.

Changamoto kubwa tunayopitia ni fedha za kujikimu halmashauri hii haijatulipa fedha za kujikimu tangu tulipoajiliwa January mwaka huu badala yake imewalipa fedha nusu watumishi wa idara ya afya pekee jambo ambalo sio sahihi na sio haki kwa watumishi tulioajiliwa nao mwaka mmoja wa ajira.

Mpaka sasa tukifatilia fedha hizo hawatupi majibu sahihi na wanatoa vitisho especially maafisa utumishi na wahasibu.

Naomba mtusaidie kupaza sauti Ili wahusika wachukuliwe hatua.
 
Back
Top Bottom