Sisi ajira mpya wa wilaya ya Nzega DC tumepewa pesa ya kujikimu tarehe 30/05/2026 kiasi cha Tsh 650,000/= badala ya 150000×7 = 1,050,000/= ukijumlisha na nauli uliyotumia wakati wa kuja kuripoti kazini.
Mbaya zaidi viongozi wetu hawasemi chochote juu ya hili, sisi tunashindwa kuelewa tupo njia panda.
Tunaomba tulipwe kiasi tunachostahili kulipwa kulingana na Miongozo iliyowekwa na serikali.