Ajira portal ina bagua baadhi ya profession

Najua sana!Underqualificaion might be a problem, but not overqualification

tatizo ni kuwa ukisha upload diploma, kuitoa inakataa, short of tht mtu ungeliweza kuitoa ukaweka certificte peke yake for that special application
Walipoweka verification ya NIDA number ndio biashara ya kuchezesha ilifika mwisho
 
Na ndio mm ninachosemea mm iloshawah kumitokea ilikuwa usaili wa afisa mipango interview tulifanya udom pale aisee jamaa walitutoa watu kibao tu
 
Hawa jamaa hamna kitu kabxa. Cha kwanza nahisi Hawa connection na taasisi zingine kama vile TCU na NACTVET. Haiwezekani Kuna kozi zinafundishwa na zinamesajiliwa ila kwenye menu yao hamna. Kwa mfano Kuna vyuo vitao higher Diploma ila wao wanasema haitambui wao wanang'ang'ania kwenye advanced diploma ambayo imefutwa kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Cha pili kuhusu mtu aliyesoma certicate -diploma -degree kama akiweka taarifa za degree hataweza kuomba tena nafasi za chini. Hii ni roho mbaya na uupuzi wa hali ya juu. Mwanzoni walikuwa wanaruhusu watu kuedit wakaja waka disable... Wanasema eti..! overqualification...! Mbona Kuna walimu wa masters na wanalipwa mishahara ya watu wa degree. Watumishi wanaweza kukijindeleza lakini mishahara hubaki pale pale labda aomba abadilishiwe Category au asubiri mpaka madaraja yapande Hadi kwenye level yake ya elimu. Kwanini wasifanye hivyo hivyo na kwenye wenye certificate na diploma waruhusiwe kuomba hata kama Wana degree zao ambayo walizipata baada ya kupitia certificate-diploma. Kuna Watu wana degree wamekaa mtaani kwa zaidi miaka 10 wamechoka, wamechakaa ile mbaya. kozi walizosoma sio marketable. Wengine wameamua kurudi chuo kwenda kusoma certificate na diploma kwa kozi zinazolipa. Wanakuja wapuuzi waliopata kazi hata bila interview wanaweka vigezo vigumu hiyo ni roho mbaya na uchawi wa hali ya juu.
 
Kwanini wasiwazuie wale waliajiriwa kujiendeleza.
 
Mkuu mbona ukiwapigia simu wanakufutiaa hiyo level kama ni ya degree na unaombaa hiyo kazii ya diploma,
 
Naomba nosaidoe namba zao mkuu
Nenda kwenye ajira portal utaonaa namba zao jaribu kupigaa zile namba zote wanapokeaga halafu uwaambiee wakufutiee degree uliwekaa bahatii mbaya wanakufutia Muda huo huo
 
Kuna Watu wana degree wamekaa mtaani kwa zaidi miaka 10 wamechoka, wamechakaa ile mbaya. kozi walizosoma sio marketable.

Mzee kozi gan izo mtu amekaa mtaani 10yrs??
 
Huoni kwamba hiyo haileti fair competition platform?

Lazima ushindanishe watu wenye sifa zinazolingana
 
Hili la level ya elimu naona ni kwa ajili ya kupanga mishahara sawa na ngazi inayohitajika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…