Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Wakuu natumaini mpo Salama:

Moja Kwa Moja niende Kwenye mada husika, kama Kichwa kinavyojieleza;

Tovuti ya Serikali ya Ajira haiweki wazi anuani ya Mamlaka au Shirika lililotangaza Nafasi za kazi Wala haitoi taarifa kwamba barua Ziandikwe kwenda kwa nani Hivyo kuweka ugumu kujua anuani ya sehemu husika.

Mara nyingi huwa najaribu kuingia katika tovuti zao lakini sio zote zinaweka Anuani na nyingine Huwa hazina Tovuti kabisa.

Mfano mzuri ni Mamlaka ya Maji safi na Mazingira Nzega (NZUWASA) amabayo wametangaza Nafasi ya Ajira lakini haijulikani Barua inaandikwa kwenda kwa nani na Anuani Yao ni ipi, Tafadhali naomba mwenye uelewa juu ya Hili anisaidie. nawakilisha
 
Niaje mkuu?
Anuani huwa ni moja tu ipo mwishoni mwa kila tangazo la kazi kutoka utumishi. Nimekuwekea hapa;

Secretary,
Presidents Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
University of Dodoma (UDOM), Utumishi Building/Asha Rose Migiro Buildings - Dodoma.
 
Shukrani sana Mkuu Kwa Muongozo, Kwa maana hiyo ni kwamba Ajira zote za Serikali nitatumia Anuani Moja tu si ndio?
 
Naombeni Msaada kwenye kipengele cha Verification Certificate, inatakiwa vyeti viwe certified na mwanasheria au na ni kila mtu lazima afanye hivyo au inakuaje.
 
Peleka kopi apige mhuri kila Cheri then scan afu ndo uwe una appload huko portal mkuu
 
Verification certificate ni category inayojazwa na watu walio soma nje ya nchi yaani vyuo ambavyo havisimamiwi na mamlaka za ndani za kielimu ndiyo huwa wana jaza hapo.

Kwa mbongo tu uliesoma hapahapa nchini jaza kawaida lakini unapoappload document yoyote hakikisha imesainiwa na wakili.
 
Napenda kufahamu kitu kimoja jamani kwenye masuala ya uandishi wa barua ya kazi utumishi.
Utumishi kwenye Ajira portal yao wanahitaji meombaji kazi aambatanishe barua ya kazzi ambayo imeandikwa kwa kingereza au Kiswahili.

Sasa issue ni kwamba, post ya Kazi husika kwenye Ajira portal imeandikwa kwa kingereza, mfano:- "Research Assistant"
Je, kama Mimi nataka kuandika barua kwa lugha ya kiswahili ninaweza kulibadilisha hilo neno Research Assistant na kulipeleka kwenye kiswahili na likakubalika/ bila kuharibu nafasi ya post husika AU inabidi niandike hvyohvyo kwenye title Hali ya kuwa barua naandika kwa Kiswahili..?
 
Fanya kama ambavyo tangazo la kazi limekuja, we utajaza kiswahili vp na post ni ya kiingereza?
 
Wadau naomba msaada: najaribu ku register kwenye ajira portal inakataa na kuniambia kuwa Email Address exists wakati sijawahi register hapa. Tatizo ni nini?
 
Wadau naomba msaada: najaribu ku register kwenye ajira portal inakataa na kuniambia kuwa Email Address exists wakati sijawahi register hapa. Tatizo ni nini?
Nina tatizo kama lako maana kuna baadhi ya vyuo hawajaorodhesha kozi zote,mfano chuo cha St.Augustine kozi za degree zote hazmo,
 
Ingia kwenye email yako pengine wameshakutumia ujumbe wa kucomfirm registration. Usipokuta fungua email nyingine
 
Ingia kwenye email yako pengine wameshakutumia ujumbe wa kucomfirm registration. Usipokuta fungua email nyingine
nataka ku register kijana wangu ana certificate in agricultre. window zingine zinagoma na hazinipi option ya kozi. na Chuo alichosoma hakiko listed katika Institutions name. Nifanyeje please
 
nataka ku register kijana wangu ana certificate in agricultre. window zingine zinagoma na hazinipi option ya kozi. na Chuo alichosoma hakiko listed katika Institutions name. Nifanyeje please
Email moja inatumika mara moja tu kufungua akaunti moja. So endapo inakataa tambua kuwa ishatumika na hivyo unapaswa kufungua email nyingine uitumie pia mara moja tu.
 
Back
Top Bottom