Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Hapo kwenye kufungua akaunti mpya umetupiga kamba mzee wangu.
Anyway, kitu unachoweza kufanya kwenye academic qualifications ni kubadilisha cheti tuu hayo mengine huwezi kubadili, yani qualification inaweza kuwa ni degree lkn cheti ukaweka cha hotel management 😎
 
Hiyo changamoto inawakuta wengi yan hiyo portal haikubali ufute cheti kabisaaa kwny academic qualification
 
Habari za kazi wakuu naomba kuuliza inachukua muda gani ajira portal kumtumia mtu email baada ya kujiajili ili aweze kuactivate account
 
Habari za kazi wakuu naomba kuuliza inachukua mda gani ajira portal kumtumia mtu email baada ya kujiajili ili aweze kuactivate account
Mbona huwa haizidi dakika 5? Otherwise shida ya mtandao
 
Tofauti ya extra time na per diem ni nini?
Extra time Ni muda wa ziada baadhi ya taasisi ukifanya kazi muda ambao sio wa wakazi unahesabiwa masaa yako ya ziada unalipwa...ila per diem ni malipo ambayo unalipwa kwa kufanya kuudhulia mafunzo flani nje ya kituo chako cha kazi
 
Hivi kwanini ajira portal wanabana sana system ya kuomba kazi utumishi yaan mtu ana vyeti vyote kaweka kwanini wasimpe uhuru wa kuapply tu na sio kuoverqualify yaan wanafanya maisha yanakuwa magumu kabisa mtaani wakati mtu ana uwezo.kabisa wa kuomba lakini system walivyoibana sio poa kabisa.

Aisee hii kitu cjui kwann wanafanya HV na wanaona
 
Jamani hawa ajira portal ni wakatili sana, nashindwa kuwaelewa kwanini wanakuwa na ubaguzi kiasi hiki..

Soma kwa makini izo qualifications na hapo kuna kitu wameandika from any equivalent qualifications lakini wananikataa mimi wa Community Development.. kweli jamani Sociology, Law, Public Administration sio Equivalent na Community Development!!
Hawa ajira portal wanajua kukatisha tamaa watu kuhusu ndoto za kuajiriwa, Mh. Rais Samia naomba sikia kilio hiki Waziri Jenista Mhagama sikia kilio hiki mama 😢😭😭

nimeumia sana kama kijana mwenye ndoto za kuajiriwa na serikali yangu pendwa. Yatapita tu 🇹🇿 Nakupenda Tanzania.
View attachment 2249732
Aisee pole sana hii kitu inasumbua wengi sana na sijui kwaniin
 
Mliyowahi kuapply kupitia mfumo wa ajira portal mlifanyaje mkafanikiwa maana mimi nagomewa.

Lakini pia kwenye kipengele cha academic qualification Hamna option ya kufuta qualification zingine msaada wenu jaman
Hii Ni kwanin unataka kufuta maana pale kweli nishida mku
 
Uzi Mtam huu,,, mwenyewe nimeshindwa sana kuomba hzo kazi Jana ni hizohzo za SUA pale tutorial.. nikajua kuomba msaada hapa Ila ni hola...!!!
Basi nimeamua kumwachia Mungu tu tusubiri zitakazokubali Ila Frankly portal Yao yakishamba sana.. hivi wanajua Maana ya neno "Equivalent"..? Wanakera kwakweli
Tatzo awwsikilizi sisi watumiaji
 
Habari,

Wanajukwaa nna shida kidogo katika kipengele cha academic qualifications kwenye ajira portal,mara ya kwanza nlieka original documents za vyeti sasa ili kuapply inabidi nieke certified copies za vyeti,sasa nkizi upload hizo certified documents na zile original certificates zinabaki.

Je, apo ninakosea au ni sawa zinahitajika zote certified copies na original vyeti

Naombeni ushauri apo wanajukwaa[emoji1488]
Ulifanikiwaa
 
Habari zenu Wana Jamvi.
Niende Moja kwa Moja kwenye kichwa Cha habari husika kwamba "Mfumo Wa Kuajiri Kupitia Ajira Portal Uondolewe".
Kwanza mfumo huu sio rafiki kwa wahusika wanaotafuta Ajira maana mfumo unabagua hatujuia walichukua heading za fani/ Kozi kutoka Chuo gani Mfano kuna watu wamesoma na wakapewa vyeti
Bachelor of Electrical Engineering wengine wakasoma Bachelor of Science in Electrical Engineering
Zinapotangazwa nafasi Ajira mfumo unaweza kuwabagua watu hawa kutokana na Title za vyeti vyao na tunasahau kile kipengele Cha relevant qualification hakizingatiwi katika mfumo.
Kingine Mfumo umekatisha ndoto za wahitimu wengi kupata Ajira serikalini Kwanini?
Kuna watu katika stage za kusoma walianzia chini kwamaana Certificate, Diploma, Degree na kuendelea. Mfano una diploma ya Umeme ukajiendeleza ukapata degree ya Umeme maana utakua na cheti Cha diploma pamoja na degree. Unapoweka cheti Cha degree katika mfumo wa Ajira portal hutoweza kuedit na kukitoa na kuomba nafasi ya diploma kama Ajira za diploma zimetangazwa maana yake inalimit watu katika kuomba Ajira Mfumo sio rafiki Bora mfumo wa zamani wa kupeleka barua utaomba nafasi kulikana na level ya elimu yako.
Kuna Mapungufu mengi katika mfumo hasa katika Kozi zinazoendana ikitokea nafasi ya Ajira mfumo unazibagua Kozi hizo ambazo zinaendana.
Nitoe Rai katika Uwongozi wa Mfumo warekebishe mfumo katika kipengere Cha Kozi zinazofanana/relevant qualification Wote waitwe kwenye Usaili washindanishwe.
Kama kurekebishwa itashindikana Mrudishe Mfumo wa zamani Kila Taasisi, Wizara na Sekta nyingine za Serikali ziajiri zenyewe Zisihusishe mfumo wa Ajira portal Sio Rafiki Unawachelewesha vijana katika kutumikia Taifa lao pendwa la Tanzania.
Nawasilisha
Ni kweli kabsa ulichosema mfumo auko friendly kabsa cjui tufanyaje kuondoa hii Keri iwezei kufika kwaoo
 
Mfumo kufutwa ni ngumu sana kwa sababu umesaidia sana watoto wa kimaskini kupata ajira mfano mimi mwenyewe nimepata kaz kupitia utumishi sina ninae mjua nmepambana kufa na kupona mungu nae kaniona. Kikubwa mfumo ufanyiwe marekebisho na wengine waweze kuomba kaz bila shida yoyote
 
Huu mfumo unaleta fairness sanaa, kuna taasisi moja kubwa tuu ilikuwa ina ukiritimba wa kuajiri wahitimu toka chuo fulani tuu, ila baada ya huu utaratibuna wengine wa vyuo vingine walinufaika pia.

Tatizo lako una tamaa sana na huelewi mambo, kikawaida your highest level of education ndiyo inayotakiwa kuwa considered kwenye ajira. Nyie ndo wale mnaopendaga kuajiriwa kama diploma, kisha mkifika kituo cha kazi mbadili gia angani muingiziwe mishahara ya degree au masters kabisa.

Kazi nyingi z serikali ziko exclusive kabisa kwamba tunahitaji labda diploma kadhaa, ama degree kadhaa. Hawatumiagi neno "angalau awe na diploma". Hivyo malalamiko yako hayako relevant kabisa.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom