Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

hakikisha umejaza kila kipengele mfano pale ktk academic qualifications jaza na upload vyeti vyako kuanzia O level , A level na vingine, upload vyeti katika pdf format.
 
Pole sana, mifumo mingi ya serikali ni ya hivyo sana...
 
Oya mwamba,mkeka unatoka lini ? Maana Ni mwezi umepita Sasa toka tutume maombi
Kuwa na subira tu mkuu, Kuna Ajira za TRA wako na miezi mi4 Toka deadline Ila Hadi Leo hawajaitwa hvyo unaweza kuona namna gani unaweza kusugua kitaa kwa mda mrefu sana.
 
Uzi Mtam huu,,, mwenyewe nimeshindwa sana kuomba hzo kazi Jana ni hizohzo za SUA pale tutorial.. nikajua kuomba msaada hapa Ila ni hola...!!!
Basi nimeamua kumwachia Mungu tu tusubiri zitakazokubali Ila Frankly portal Yao yakishamba sana.. hivi wanajua Maana ya neno "Equivalent"..? Wanakera kwakweli
Limenikuta kwenye vigezo wameandika bachelor of education in science (chemistry) na kazi ambayo ninayo muombea mtu huyo kasoma lakini ukiomba failed piga simu hawapokei ukipiga tena inatumika ikiita hawapokei.
 
Ajira portal nafikiri wanao run hii system wamekwamisha saana ndoto za watu kupata ajira. Mfano mtu anaweza kua anaomba kazi ya uhasibu .na JD inakuainishia kozi kazaa , Lakini wao watataka mtu aliye soma account tuu wakati kuna kozi nyingi alizosoma anafanya kazi za uhasibu.

Nafikiri wapo very rigid saana hata hawabadiriki kabisa.
Hili bado limekuwa tatizo kubwa
 
Ukitaka kuchange course kuendana na tangazo (Equivalent courses) ili uweze kuapply fanya hivi, 1 nenda sehemu ya academic qualifications 2 nenda sehemu ya saved academic qualifications ( kwenye cheti cha chuo) utakuta sehemu mbili, ya attachment na EDIT, wewe utabonyeza kwenye EDIT baada ya hapo itakupeleka kwenye taarifa zako za chuo utaenda kuedit sehemu ya PROGRAMME NAME ( course uliyosoma au inayoendana nahiyo). Baada ya hapo utabonyeza sehemu ya save. Baada ya hapo utarudi kwenye kazi unayotaka kuapply na utaapply bila shida.

sijaweka maneno,ninaandika 3.8 ndio inasoma hivi
Hapo hata me mwenyewe unanivuruga.. mbona watu wanaandoka tu hapo na inakubali..
Waface kwa Email Yao watakusaidia chap
 
Vipi wakuuu
Ishu ya kuverify vyeti unaifanya kila unapoomba ajira?

Au unafanya mara moja for lifetime
 
Kama ushaweka verified/certified Haina shida..
Kaka kuna mtu ni wa hapa bara ila kwenye kujaza amekosea ameweka origin ni tanzania-zanzibar badala ya main land,je hii itaathiri maombi yake?,
maana hii sehemu haikubali editting;

Pia naomba kujua,hivi inatakiwa kuweka chet cha kumaliza form four (form four leaving certificate) na kile cha kumaliza form six (form six leaving certificate) ?,
 
Back
Top Bottom