Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ni
Mfumo kufutwa ni ngumu sana kwa sababu umesaidia sana watoto wa kimaskini kupata ajira mfano mimi mwenyewe nimepata kaz kupitia utumishi sina ninae mjua nmepambana kufa na kupona mungu nae kaniona. Kikubwa mfumo ufanyiwe marekebisho na wengine waweze kuomba kaz bila shida yoyote
Kweli mzee kule amna upendeleo ila naona pale kwenye academic wamerekebisha tofaut na mwanzo
 
Changamoto #2 naiona sio changamoto kabisa.
Unajua mtu akiwa na njaa ya ajira hata akiwa na PhD ukimwambia nitakulipa laki 4 anakubali.
Ukimwajiri tu akizoea mazingira ataanza kuona anaonewa, ataanza kupoteza morali, ataanza kuibia serikali kwa hasira.
Atasema nalipwa mshahara mdogo kuliko elimu yangu, kuna watu tuko na level moja ya elimu au nimewazidi lakini wanalipwa ndefu.
Haya umeajiriwa kwa certificate lakini una diploma, na degree kabatini, na kazini supervisor wako aidha ana degree au diploma utajisikiaje?
Serikali ina akili kuliko wewe
 
Tatizo sio Portal..., Tatizo ni Hizo Ajira hazitoshi / hazikidhi mahitaji; unadhani demand ingekuwa kubwa kuliko supply wangetoa hata pesa na ku-advertise kwenye maluninga, matovuti na sms hata wale wasio na simu janja au vishikwambi waweze kujisetiri....

Yaani wewe sio kuomba tena / Kuapply bali ni kubembelezwa; ila ndio hivyo tena....
 
Habari zenu Wana Jamvi.
Niende Moja kwa Moja kwenye kichwa Cha habari husika kwamba "Mfumo Wa Kuajiri Kupitia Ajira Portal Uondolewe".
Kwanza mfumo huu sio rafiki kwa wahusika wanaotafuta Ajira maana mfumo unabagua hatujuia walichukua heading za fani/ Kozi kutoka Chuo gani Mfano kuna watu wamesoma na wakapewa vyeti
Bachelor of Electrical Engineering wengine wakasoma Bachelor of Science in Electrical Engineering
Zinapotangazwa nafasi Ajira mfumo unaweza kuwabagua watu hawa kutokana na Title za vyeti vyao na tunasahau kile kipengele Cha relevant qualification hakizingatiwi katika mfumo.
Kingine Mfumo umekatisha ndoto za wahitimu wengi kupata Ajira serikalini Kwanini?
Kuna watu katika stage za kusoma walianzia chini kwamaana Certificate, Diploma, Degree na kuendelea. Mfano una diploma ya Umeme ukajiendeleza ukapata degree ya Umeme maana utakua na cheti Cha diploma pamoja na degree. Unapoweka cheti Cha degree katika mfumo wa Ajira portal hutoweza kuedit na kukitoa na kuomba nafasi ya diploma kama Ajira za diploma zimetangazwa maana yake inalimit watu katika kuomba Ajira Mfumo sio rafiki Bora mfumo wa zamani wa kupeleka barua utaomba nafasi kulikana na level ya elimu yako.
Kuna Mapungufu mengi katika mfumo hasa katika Kozi zinazoendana ikitokea nafasi ya Ajira mfumo unazibagua Kozi hizo ambazo zinaendana.
Nitoe Rai katika Uwongozi wa Mfumo warekebishe mfumo katika kipengere Cha Kozi zinazofanana/relevant qualification Wote waitwe kwenye Usaili washindanishwe.
Kama kurekebishwa itashindikana Mrudishe Mfumo wa zamani Kila Taasisi, Wizara na Sekta nyingine za Serikali ziajiri zenyewe Zisihusishe mfumo wa Ajira portal Sio Rafiki Unawachelewesha vijana katika kutumikia Taifa lao pendwa la Tanzania.
Nawasilisha
Nakwambia ni disaster
 
Kama umewahi kufanya application ya maombi ya kazi kupitia mfumo wa ajira portal utakubaliana na mimi huu ni mfumo wa kijinga sana kuwahi kutokea

Just imagine wametangaza nafasi za kazi za Tutoria Assistant(Accounting and Finance). Wanataka mtu aliesomea ACCOUNTING AND FINANCE or BUSINESS ADMINISTRATION IN ACCOUNTING AND FINANCE, kama inavyoonesha hapa chini;

Screenshot_20221013-114446_Chrome.jpg


Sasa mtu amesomea chuo Bachelor of business administration in accounting na mfumo unakukubali kuomba kazi unaomba, mwisho wa siku wanakuja kusema hauna qualification na wakati G.P.A iko sawa kisa tu iyo finance😭😭

Screenshot_20221013-114420_Chrome.jpg


Halafu unawapigia simu wanasema mtu unakua umeucheat mfumo wakati vyeti na kila kitu umewawekea, how can this be possible..huu mfumo wa portal ni wa kipumbavu...otherwise hizi changamoto zinakatisha ndoto za watu wengi na ukizingatia majina yenyewe wanachelewa kuita watu.
 
Kama vile ambavyo wanafunzi wanaosoma vyuoni kushindwa kuelewa kwamba unaweza kupata kazi kwa kutumia hata module moja tu..ndivyo hivyo hivyo hao watu wa PSRS wanavyokariri kwamba lazima usome accounting nkt hata mtu aliesoma Finance kuna maswala yanamuwezesha kufanya..kwenye accounting
 
Kama vile ambavyo wanafunzi wanaosoma vyuoni kushindwa kuelewa kwamba unaweza kupata kazi kwa kutumia hata module moja tu..ndivyo hivyo hivyo hao watu wa PSRS wanavyokariri kwamba lazima usome accounting nkt hata mtu aliesoma Finance kuna maswala yanamuwezesha kufanya..kwenye accounting
Ni wajinga sana mkuu
 

Udhaifu, Maoni na Mapendekezo kwa Tume ya Ajira "PSRS"
 

Udhaifu, Maoni na Mapendekezo kwa Tume ya Ajira "PSRS"
Asante mkuu labda mods wataangalia namna gan wauweke uzi wangu kwenye post yako maana hata mimi nimepiga simu kapokea mdada ambaye kabisa ni kama hajui anachokisema..kuna haja hata ya makatibu siku moja moja kupiga simu za hao jamaa waone watu wao walivo hawana weledi na majukumu yao..iyo system ya kishenzi na kipuuzi
 
Ushauri wa bure..kama una umri wa miaka 30 una degree yako ni mwaka wa 3 unatafuta ajira hujaipata achana na hizo ishu unapoteza muda, kuna umri ukifika watu hawatotaka kujua umesoma mpaka wapi ila wao watataka waone maendeleo yako tu...........
 
Wakuu naombeni msaada, kila ninapojaribu ku update picha naona ina load tu lakini haibadiliki.

Picha iliyopo sasa hivi niliiweka wakati nipo certificate, sasa haikuwa ya passport size ilikuwa ni picha ya kawaida tu ya photo shoot.

Kwa anaejua namna ya ku update picha nyingine naomba anisaidie maana kila nikijaribu inagoma, msaada wakuu tafadhali.
 
Wakuu naombenisaada kila ninapo jaribu ku update picha naona Ina load tu lakini haibadiliki. Picha iliyopo saizi niliiweka wakati nipo certificate Sasa haikua ya passport size ilikua ni picha ya kawaida tu ya photo shoot. Kwa anaejua namna ya ku update picha nyingine naomba anisaidie maana kila nikijaribu inagoma msaada wakuu tafadhari
Subiri usiku mtaandao ukikaa vizuri jaribu tena hapo ni ishu ya network tu wala sio kingine
 
Wakuu naombenisaada kila ninapo jaribu ku update picha naona Ina load tu lakini haibadiliki. Picha iliyopo saizi niliiweka wakati nipo certificate Sasa haikua ya passport size ilikua ni picha ya kawaida tu ya photo shoot. Kwa anaejua namna ya ku update picha nyingine naomba anisaidie maana kila nikijaribu inagoma msaada wakuu tafadhari
na huenda ushaiupoad sema hiyo search engine ndo inakupa huo mrejesho.

fanya hivi tumia search engine nyingine kulogin kwa mf..kama ulisearch na samsung internet/google now tumia chrome then login...!

Au tumia device nyingine kulogin.Kama ulitumia simu yako kusearch(kuplload) now tumia simu/laptop nyingine kulogin.

then, lete mrejesho.
 
na huenda ushaiupoad sema hiyo search engine ndo inakupa huo mrejesho.

fanya hivi tumia search engine nyingine kulogin kwa mf..kama ulisearch na samsung internet/google now tumia chrome then login...!

Au tumia device nyingine kulogin.Kama ulitumia simu yako kusearch(kuplload) now tumia simu/laptop nyingine kulogin.

then, lete mrejesho.
Shukrani mkuu itabidi nijaribu njia hii nikifanikiwa ntaleta mrejesho ndugu
 
Back
Top Bottom