Ajira za bara tunaomba wote, lakini za Zanzibar wanataka Mzanzibar pekee
Kuwa tu mpole. Maana viongozi wetu wa Tanganyika, wakiwa na akili zao timamu wamekubali tuwe na Muungano wa hovyo kabisa wa changu changu, chako changu na hao Wazanzibari.
Babu wewe ni mchoyoo utaona lakini ipo siku yako 🤣🤣🤣🤣
 
Serikali inapaswa kutafakari ni kwa namna gani wanaweka usawa kwenye hili.

Wahitimu kutoka bara wanalalamika sana. Ajira zinazotangazwa bara wanasailiwa hadi wazanzibar, lakini ajira zinazotangazwa Zanzibar, sifa moja wapo kubwa ya kusailiwa ni kuwa mzanzibar.

Mzanzibar anafaida mara 2, anaweza kupata ajira Zanzibar au Bara. Hii ipo tofauti kabisa kwa wahitimu wa bara.

Serikali wanaweza kuchukulia swala hili kama swala dogo sana, ila kiuhalisia linakuza chuki ndani ya muungano wetu. (Ajira ni moja ya changamoto kubwa tena inagusa kundi kubwa yaani vijana).

Serikali kupitia ofisi wa makamu wa Raisi, wizara ya kazi pamoja na utumishi wanatakiwa wakae na kuchukua hatua za haraka mapema. Baada ya miaka kadhaa hili swala litakuwa kubwa na halitaweza kutatulika kirahisi.
Kamsome mzee Mohamed said wa jukwaa la historia vizuri bila kujali itikadi utapata jibu mujalabu
 
Mmesoma wote chekechea mpaka chuo Tanania bara lakini wao hupewa kipaumbele kwenye ajira kwa kigezo cha kubalance muungano

Mmeenda wote mafunzo ya jkt, wao wana asilimia kubwa ya kuajiriwa moja kwa moja kwa kigezo cha kudumisha muungano

Akikosa ajira Bara anaweza kwenda Zanzibar
 
Zanzibar inatekeleza mkakati wa kukontro population isiongezeke kwa kasi mana kisiwa kile kina limited space
 
Back
Top Bottom