NAKUKUNDA TANZANIA
Member
- Jun 17, 2024
- 12
- 14
Tangu kuanzishwa kwake, Tume ya utumishi wa mahakama imekuwa ikiajiri mahakimu kwa kufuata utaratibu wa michujo na kuwachagua wale waliofuzu kwa vigezo stahiki kupitia tangazo maalumu na la wazi.
Lakini tarehe 20 Septemba 2024 Jaji Mkuu wa Tanzania, aliwaapisha mahakimu 22 ambao baadhi yao hawajulikani wametoka wapi na wamechaguliwa kwa vigezo gani! Uchaguzi wao ulikuwa wa mficho bila taarifa kwa umma.
Hata majaji wanapoteuliwa na Rais huwa wanatangazwa na kuapishwa kwa uwazi, kwanini hizi ajira za mahakimu zimefanywa kwa uficho tarehe 20 Septemba 2024?
Natoa wito kwa mamlaka husika kumulika tochi zao kuona nini kilifanyika.