Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. EZRA CHIWELESA - AJIRA 21,200 KILA HALMASHAURI INAWEZA KUPATA WATUMISHI WAPYA 115 KAMA ZIGAWIWE KWA USAWA
Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa ameunga mkono hoja na kuchangia katika bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora.
Mhe. Chiwelesa amesisitiza uwazi na ugawaji sawa wa nafasi za ajira zinapotoka kwani kati ya Nafasi 21,200 zilitolewa na TAMISEMI kila Halmashauri inaweza kupata wafanyakazi wapya 115.
Mhe. Chiwelesa amesema Serikali itumie busara kuwaangalia vijana waliohitimu vyuo vya Utalii wenye umri zaidi ya miaka 25 ambao jeshi halikuwaajili kwa kigezo cha kuzidi miaka 25 kwani wanaujuzi na wazazi wao walitumia gharama kubwa kuwasomesha.
Mhe. Chiwelesa amesisitiza pia kuwa ajira za sekta zingine za TRA, TANESCO, BoT n.k pia ziwekwe wazi wakati wa mchakato wa kuwapata watumishi kama ilivyo kwa TAMISEMI. Kwani kumekuwa na tabia ya kuangalia undugu, ukabila na watoto wa viongozi katika sekta mbalimbali.