Ajira za utotoni: Sheria inawalindaje watoto katika hili?

Ajira za utotoni: Sheria inawalindaje watoto katika hili?

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Habari za muda wakuu. Katika pita pita zangu nimekutana na hii Sheria, kuna baadhi ya vitu najiuliza. Naomba muongozo kutoka kwa ndugu zetu wataalamu wa sheria.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Kazi, 2004, mtoto chini ya miaka 14 hapaswi kuajiriwa. Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu, ambazo haziwezi kuwa na madhara kwa afya ya mtoto na maendeleo yake”.

Sehemu nyingine imeeleza kuwa:

"Mtoto haruhusiwi kufanya kazi wakati wa saa za shule. Na mtoto anaye endelea na masomo, haruhusiwi na hapaswi kufanya kazi kwa zaidi ya masaa matatu kwa siku. Mtoto wa umri wa miaka 14 na zaidi na anapokuwa likizo au amekwisha hitimu elimu ya msingi, au hasomi kwa sababu mbali mbali za msingi, anaweza kuajiriwa kufanya kazi kwa kipindi kisicho zidi masaa 6 kwa siku. Mtoto asiruhusuiwe kufanya kazi kwa masaa matatu mfululizo bila ya walau saa moja ya mapumziko".

1. Je, Watoto (walio chini ya umri wa miaka 18) wanaofanya kazi za ndani wanalindwa vipi? Wengi hao wamekatisha masomo na wanafanya kazi siku nzima. Kisheria, hii imekaa vipi? Sheria inawalinda vipi Watoto hawa?

2. Kwa mfano nipo katika mazingira ambayo nashuhudia mtoto anafanya kazi katika mazingira magumu, ni hatua gani naweza kuchukua kumsaidia? Naanzia wapi kisheria kuhakikisha Sheria inachukua mkondo wake?

3. Wazazi na wanaoajiri Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wanawajibishwa ipasavyo? Kwa sababu nafasi yao katika kumkosesha mtoto haki yake ya msingi ni kubwa.

Nakaribisha wataalamu kwa ufafanuzi zaidi.

Shukrani.
 
beth,
Ukiona tukio la ukatili dhidi ya watoto piga 116 bure wakusaidie.

Kuhusu sheria inamlinda vipi mototo afanyaye kazi za ndani na kumuwajibisha mzazi ama mtu yoyote anayemkatili, mbali na kifungu ulichoainisha, kimsingi sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inaangalia ustawi bora wa mtoto yaani 'best interest of the child' katika jambo limhusulo mtoto yoyote.

Changamoto ni utekelezaji wa sheria, mfano kama mwananchi mtu mzima hajui ni wapi pa kuanzia kupeleka malalamiko dhidi ya mtoto anayefanyiwa ukatili ili sheria ichukue mkondo wake, je mtoto atafanyaje?
 
kumuajiri mtoto afanye kazi za ndani ni kinyume cha sheria. Ieleweke hivyo tu.

Ndio maana wengi huwaita ni watoto wao.
 
Back
Top Bottom