Ajira za walimu 36,000 kumwagwa mwaka huu

Ajira za walimu 36,000 kumwagwa mwaka huu

Majina ya vituo vya kazi yanategemewa kuitoka katikati ya mwezi huu na kuripoti April mos...source gazeti nipashe la Leo ukurasa wa 8 pia taarifa ya naibu waziri Tawala za mikoa na serikali za mitaa Elimu Kasimu Majaliwa akizungumza katika kipindi cha kumepambazuka Jana cha redio one...Hebu tuvute Subira walimu wenzangu tuone hyo katikati ya mwezi huu ambayo haikutajwa tarehe....

sawa lets wait
 
jidanganye tu

ha ha ha,ndo ukweli huo mkuu,sasa mtoto wa bcom au economics akafanyaje bush na wakati michongo yake yote iko town kwenye ofisi nzuri na zenye viyoyozi?
 
Majina ya vituo vya kazi yanategemewa kuitoka katikati ya mwezi huu na kuripoti April mos...source gazeti nipashe la Leo ukurasa wa 8 pia taarifa ya naibu waziri Tawala za mikoa na serikali za mitaa Elimu Kasimu Majaliwa akizungumza katika kipindi cha kumepambazuka Jana cha redio one...Hebu tuvute Subira walimu wenzangu tuone hyo katikati ya mwezi huu ambayo haikutajwa tarehe....

Huyu kassim majaliwa aanaataka sana uumaarufu mara nyingi anaropoka tu pasipo na ukwelli, last three weeks alikuja na taarifa kuwa internal auditos wataanza ku-repot kwa CAG, kwaa mtu anayeelewa ni kukangaanyana dhana nzima ya stewardship ambayo kimsingi ndio inaaleta dhana ya uwajibikaji. Siku chache tu CAG alkanusha kaulii hiyo.

Kwa kifupi nahic anataka apite upande mwingine kupata umaarufu kama wa Aggrey Mwamri.

Kwa hiyo bado kauli hiyo ya ajira ya walimu siyo reliable kwa sababu ya kiongozi ambaye amekuwa anatoa matamko yasiyo sahihi kwa kutaka sifa asizostahili!!
 
Na ikumbukwe huyu jamaa alipishana na mkuu wa kaya kuhusu idadi ya watakao ajiriwa.

Pia alinukuliwa Morogoro akisema ajira zitatolewa mwezi wa kwanza.
 
Kassim%20Majalliwa%20.jpg

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa.

Serikali imetangaza kuwajiri walimu wapya 36,071 mwaka huu ambao majina yao yanatarajia kutangazwa katikati ya mwezi huu (Machi) na watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi Aprili mosi mwaka huu.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa, aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka jana kinachorushwa na Radio One.

Majaliwa alisema walimu hao watapangiwa katika vituo mbalimbali vya kazi kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu na majina yatatoka katikati ya mwezi huu.

Alisema kati ya walimu hao watakaoajiriwa, 36,020 wataajiriwa na halmashauri za wilaya ambao ni walimu wa shule za msingi na sekondari na 51 watakuwa chini Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya vyuo.

Aliongeza kuwa kati yao, walimu wa stashahada ni 17,028 na 5,416 ni wa shahada kwa ajili ya sekondari na 12,677.

Alifafanua kuwa wanaoajiriwa ni wale waliohitimu hivi karibuni katika vyuo vya ualimu na walimu wa masomo ya sayansi watapewa kipaumbele.

Majaliwa alisema tayari Wizara imewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri na maofisa elimu kupitia ikama ya walimu kubaini shule zenye upungufu wa walimu ili walimu hao wapya wanaoajiriwa wapelekwe huko hususani katika shule zilizopo vijijini.

Alisema kuajiriwa kwa walimu hao kumepunguza tatizo la upungufu wa walimu 21,684 baada ya ajira hiyo na kwamba hata hivyo upungufu mkubwa kwa walimu wa sayansi ni 26,212.

Alisema serikali imeweka mkakati wa kukabiliana na tatizo la punguza wa walimu wa sayansi kwa kuwachukua wanafunzi waliohiotimu vyuo vikuu ili wapelekwe kwenye vyuo vya ualimu.

Kuhusu tatizo la baadhi ya walimu kukimbia vituo vya kazi, alisema kimsingi sheria ipo wakishaajiriwa wanakuwa katika kipindi cha matazamio cha miaka mitatu na wanafanyiwa ukaguzi na wakaguzi ili kubaini kama wana uwezo wa dhati.

CHANZO: NIPASHE
 
Wanataja katikati ya mwezi huu!wanafikiri mbaliii! let us wait!.
 
Naona wanacheza na hesabu na sio hali halisi, mda wote waliokaa bila kuajiri walidhani watu wataishi vipi?

Idadi kubwa hivi sasa hasa walimu wa sayansi tayari wamesha saini mikataba shule za private.

Wanasema wanaajiri 36 elfu hali halisi watakao patikana ni 50%.

Serikali inabidi iangalie suala hili, kama kweli inauhaba wa walimu na inahitaji kuelimisha watu wake basi ni vema wakawa washindani katika soko.

Inatakiwa wawe wanaajiri walimu mara anapomaliza chuo.

Katika taarifa hii ya Majaliwa nilitegemea aanze kuomba samahani kwanza kwa kudanganya umma wa watanzania, nnakumbuka alisha wahi kunukuliwa kwenye gazeti la HABARI LEO akisema ajira zingetolewa mwezi wa kwanza lakini haikuwa hivyo.

Tulikuamini Majaliwa 100% mara ya kwanza lakini kwa hivi sasa tunakuamini kwa 50%, atoe ajira kama alivyosema ili angalau tuanze kumuamini tena.
 
Nnaimani taarifa za

1. Akina baba mdogo.

2. Watu walio jikoni

hazina nafasi, walipewa nafasi ya kuonesha uaminifu wao wameshindwa.
 
majanga ma2pu siamini tena kwenye tetesi kauli k2 gani mara ngap wametangaza????tangu january had leo npo zangu private nakula bata mie serikali yangu ni kichwa changu tu!!!!
 
Kasimu kwani ukitoa majina leo watu wajue wamepangiwa wapi kuna tatizo gani?
Kila mara unatangaza ajira majina hatuyaoni!
Siamini pia mwez huu kama usemacho ni kweli.
 
Mr.Thobias nadhani umechanganya idadi,idadi sahh ni stashahada ni 5,416,shahada ni 12,677, cheti ni 17,928 na vyuo ni 50.
 
Mr.Thobias nadhani umechanganya idadi,idadi sahh ni stashahada ni 5,416,shahada ni 12,677, cheti ni 17,928 na vyuo ni 50.

Thats correct! Tafadhar watoa mada muwe makini mnapotoa thread zenu! Hzi habari siye wengne tunatumia kama 'refferences' sasa mnapokosea mnatupoteza! fyuuuu..,...
 
Thats correct! Tafadhar watoa mada muwe makini mnapotoa thread zenu! Hzi habari siye wengne tunatumia kama 'refferences' sasa mnapokosea mnatupoteza! fyuuuu..,...

Vp baba mdogo hajakupa fununu za tarehe rasmi ya kutoa majina?
 
Back
Top Bottom