mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Imekuwa ni kawaida kuona figisu figisu ikitawala katika ajira za walimu. Baadhi ya figisu figisu hizo ni kama ifuatavyo.
1. Kutangazwa kwa nafasi za walimu wa Physics na Hesabu lakini wakachaguliwa baadhi ya walimu wa biology na chemistr. Walimu wa chemistry na biology ambao hawakuomba wakaona wamepigwa chenga ya mwili.
2. Mwalimu mmoja jina lake kutoka zaidi ya mara mbili. Matukio ya namna hii yalikuwa kwenye idadi amb ayo si rahisi kuona kuwa ni bahati mbaya. Inaonekana kuna nafasi zimehifadhiwa kwa baadhi ya watu ambao hawakuwa na sifa za kuchukuliwa moja kwa moja.
3. Kuajiriwa walimu ambao wamemaliza chuo juzi wakati walimu waliohitimu miaka mingi iliyopita wa masomo hayo hayo wakiwa wameachwa.
ongezeeni zingine!
Tuseme mapema safari hii tutawekeana pingamizi mahakamani kama uozo kama huo utajirudia. Na ni lazima uwepo uwazi wa hali ya juu kuhusu vigezo vinavyopimika vitakavyotumika.
Kigezo kimoja kisichokuwa na upendeleo ni wa foleni kwa masomo husika. Yaani waliohitimu mwanzo wachaguliwe kwanza.
Hiyo itafanya waliobaki wawe na amani huku wakijua angalau nao wamesogea kwenye foleni. Lakini ukiajiri wahitimu wa hivi karibuni na kuwaacha wahitimu wa miaka ya nyuma kwa masomo yale yale inavunja moyo na kukatisha tamaa swana.
Wakubwa tunawaomba wasithubutu kusumbua watendaji kwa vimemo!! Ningeshauri mkubwa yeyote akisumbua na kimemo, utaratibu ufanyike wa kukianika hapa Jf na mitandao mingine ya kijamii.
Hiyo itakuwa ni adhabu kubwa sana kwake na tutamwomba mama amtengue!! Takukuru na vombo vingine vya dola iweni macho kwa hili.