Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nauliza tu maana nina utata. Kama tulikuwa hatuajiriwi Zanzibar kwenye mambo yaliyochini yao je Wazanzibari walioajiliwa kwenye mambo yaliyokuwa ya muungano zamani watarudi kwao? Nisadieni utata huu
Na kwa sasa suala la uraia wa nchi mbili halikubaliki itabidi wachague moja. Nilivundua hilo wakati wa ugawaji viwanja geza nusu ya waombaji ni wapemba. Nenda kibada nusu ya viwanja vyote vya barabarani ni waoKiukweli hata sasa wamejazana huku bara hadi kwenye halmashauri zetu.
Nauliza tu maana nina utata. Kama tulikuwa hatuajiriwi Zanzibar kwenye mambo yaliyochini yao je Wazanzibari walioajiliwa kwenye mambo yaliyokuwa ya muungano zamani watarudi kwao? Nisadieni utata huu
Rasimu tu watu wanapagawa,vipi itakapokuwa kamilifu itakuwaje?
Ajira za nini tena! Tukutane kwenye serikali ya shirikisho tu, wazanzibar waendeshe serikali Yao na watanganyika pia waendeshe serikali Yao, Hakuna kumiliki ardhi kwa wazanzibar bara na watanganyika Zanzibar, Mia.
Halafu umenikumbusha mkuu, hivi suala la ardhi vipi tumeamuaje kwenye rasimu? Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata nafasi ya kuisoma rasimu yote. Je wazenji itabidi watuachie ardhi au watanganyika tutakuwa ruksa nasi kwenda kujenga nyumba kibanda maiti,dole,mchamba wima,kijito uvivu etc?
Hilo litategemea sheria zetu, anzeni kupeleka maombi kupitia kwa waziri wenu mkaazi (resident minister) ofisi yake itakuwa Tunguu mkabala na Chuo Kikuu Cha Taifa, ANGALIZO hamtakuwa na haki ya kumiliki ardhi, mpaka nyumba mutakazojenga zimilikiwe kwa pamoja 50/50 na mzanzibari, meaning nyumba itakuwa ya kwako lakini ardhi ya mzanzibari, ataamua kiasi cha kodi ya ardhi utakacholipa kwa mwaka.
Nyumba za wazanzibari zilizopo bara zimejengwa kabla ya uhuru wa mara ya pili wa Tanganyika, so you can't do nothing, vinginevyo, we will meet at East African Court of Justice or The Hague. Serikali ya Zanzibar inakusudia kupeleka mswada Baraza la Wawakilishi kabla ya 2015 kuanzisha mfuko maalum wa kuendesha kesi dhidi ya uzalilishaji wa wananchi wake watakaoamua kuishi mrima. tunategemea kuajiri mawakili wenye uwezo mkubwa kutoka Nigeria kwa ajili ya kazi hiyo akiwemo Prof. Swanzi.
Mkuu wale wachina wanao chimba dhahabu tanganyika wameomba uraia?punguza jazba.Unachekesha kweli wewe, hata mjerumani alijenga nyumba Tanganyika yote kabla hata Tanganyika haijapata uhuru lakini nyumba hizo sasa hivi zinamilikiwa na nani? Sasa kama wewe huna uraia wa Tanganyika uhalali wako wa kumiliki hiyo nyumba utatokea wapi? Pili Ardhi ya Tanganyika ni mali ya serikali ya Tanganyika tutawalipa fedha ya urojo tu halafu nyumba zinarudi kwenye himaya yetu. Vinginevyo uombe uraia wa Tanganyika.
Mkuu wale wachina wanao chimba dhahabu tanganyika wameomba uraia?punguza jazba.