Boyfriend15
Member
- Jul 22, 2022
- 45
- 102
Habari za muda huu wakuu,
Nipo mbele yenu kutoa ushuhuda wa jinsi jukwaa hili lilivyoleta mwanga kwenye maisha yangu.
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa hapa nilipo naamini kusudi lake na matakwa yake yamenifanya nifike hapa leo hii.
Mimi ni kijana nilimaliza degree yangu ya accounting and finance in business sector chuo kikuu mzumbe, ndaki ya mbeya mwaka 2023.
Maisha baada ya kumaliza chuo hayakua mepesi kabisa,ukizingatia mimi natoka katika familia ya tabaka la chini kiuchumi na ndio mtoto pekee ambae katika familia ambae nimepata degree,kwahiyo familia yote ilikua ikiniangalia mimi kama mkombozi, na mbaya zaidi tayari nilikua nimejichanganya nikiwa mwaka wa tatu chuo kuna demu niliteleza nikampa mimba so ninavomaliza chuo tayari mimba yake ilikua ina kama miezi 2 hivi,
Baada ya kumaliza chuo, nilifanya maamuzi magumu ya kuamua kubaki geto na sio kurudi nyumbani kwani sikutaka kwenda kuongeza mzigo nilijipa moyo kupambana na maisha kama mwanaume.kusema ukweli maisha baada ya chuo yalikua magumu sana ukizingatia presha ya kuwa mtoto ambae familia inanitegemea kwa kila kitu, na presha kutoka kwenye familia ya huyo mwanamke ambae alikua na ujauzito wangu (familia yake ilikuwa inakuja juu sana kipindi hiki walikua na makasiriko sana)plus presha ya gharama za malezi ya mimba mpaka kujifungua na sikua na kazi yeyote ambayo ingeweza kunipa unafuu wa maisha, nilihisi kama dunia inanielemea.
Ndipo nilipoamua kuja kuomba msaada wa kibarua chochote humu jamii forums chapisho langu lilikua hili hapa
Thread 'Sitaki kufa njaa kitaani'
Sitaki kufa njaa kitaani
Lakini sikufanikiwa kupata kazi yeyote kitaa kilikua kigumu sana maisha yalinichapa ile mbaya, katika kuhangaika huko na huko nikapata wazo la kuhama mbeya na kuhamia dar es salaam nikiamini dar kuna kampuni nyingi kubwa hivo ingekua rahisi kupata kazi kuliko kukaa mbeya, basi nilifunga safari mpaka dar kupitia lori ambalo jamaa mmoja tulisoma nae o level ndio alikua dereva anapiga route ya zambia dar so nikampanga kisha nikadandia lori mpaka dar, dar nilifikia kwa rafiki angu mmoja pugu huko, lakini mambo yakawa kinyume na matarajio kwani bado nilikosa ajira nikatamani hata kutafuta experience kwa kujitolea nikarudi tena humu jf na kuandika chapisho hili.
Thread 'Kwani hamtaki watu wa kujitolea?'
Kwani hamtaki watu wa kujitolea?
Hapa nilibahatika kupigiwa simu kazaa na kuhaidiwa ahadi zilizoota mbawa.
Nilisota sana dar niliona chungu, nikiendelea kutafuta kazi bila mafanikio nikituma cv na kuzunguka makampuni mengi kuomba kujitolea lakini ilishindikana kusema ukweli nilihisi kukata tamaa.
Siku moja nikiwa napita pita jf nikaona tangazo la MOST WANTED hili hapa ilikua tar 17/01/2024
Thread 'Accountant/Muhasibu Anahitajika'
Accountant/Muhasibu Anahitajika
Mhasibu alikua anahitajika katika construction company iliyopo mbeya kwa haraka, nikampm lakini kwa bahati mbaya tayari alikua ashpata mtu ambae ni mdada na alikua anaenda kwenye interview kesho yake, basi niliaminihaikua ridhiki yangu, lakini baada ya siku kama 3 hivi most wanted alinirudia na kunambia kama naweza kuapatikana yule dada kuna mazingira yalimbana na kushindwa kuifanya kazi, nakumbuka sikuwa hata na mia mfukoni halafu nilitakiwa kurudi mbeya haraka kwaajili ya interview ambayo nayo sikuwa na uhakika wa kupata kazi, lakini kwa imani nikaamua kutake risk nikahangaika kukopa nauli nikafanikiwa kupata kwa demu mmoja hivi alikua mshkaji wangu sana basi nikarudi zangu mbeya nikapiga interview.na kwa uwezo wa mungu kupitia tangazo hili nilifanikiwa kupata kazi baada ya hustle ya muda mrefu. Japo haikua na malipo makubwa ya kutosha hata nusu ya mahitaji yangu lakini kidogo ilileta auheni.
MOST WANTED nashukuru sana brother mungu akubaliki sana
Baada ya kupata kazi na kusaini mkataba na kampuni hii ya ujenzi basi ni kama ilifungua milango nilipata simu kama nne hivi kutoka katika kampuni ambazo nilikua nimeshare cv na nyingine kufanya interviews kipindi natafuta ajira, tena kukiwa na malipo mazuri nakumbuka moja ya kampuni ofa yao ilikua ni mara 3 ya ninachokipokea katika kampuni niliyokua nafanya kazi.ilikua ni mapema mno hivyo niliweka tamaa pembeni na kuamua kureject ofa zote, nikiamini katika kujenga cv licha ya kuwa na hali mbaya kiuchumi. Nimefanya kazi katika kampuni hiyo kwa karibia mwaka 1 na miezi 2 nikijituma na kufanya kwa weledi.
Baada ya kujenga cv na kuona sasa ninaweza kutafuta changamoto mpya ya kukua zaidi katika taaluma yangu ndipo nikaanza kutafuta upya kazi huku nikiangalia maslahi na mazingira ya kazi, nilplan strategies ambazo niliamini zingeweza kunisaidia kupata kazi kwa urahisi ikiwemo kutengeneza profile zangu vizuri za mitandao ya kijamii, pia nikajiunga na hawa recruitment agency (siku nitakuja na thread special kuhusu strategies hizi na hizi recruiting agencies za tanzania).
Siku moja mwanzoni mwa mwezi wa 3 mwaka huu kupitia hawa recruiting agency nilipigiwa simu ya kuitwa kwenye interview katika Ngo moja kubwa hapa Tanzania nilifanya interviews kama nne hivi, na nilifanikiwa kusecure nafasi na nikapata ajira ambayo mshahara wake umechangamka na alhamdulillah sasa naweza kumudu maisha yangu na ya familia yangu sio kama mwanzo.
Vijana wenzangu na wanajukwaa wote kwa ujumla Inawezekana kuna mtu anapitia maisha niliyopitia au tofauti na yangu lakini kama upo katika utafutaji wa ajira usikate tamaa, kikubwa ni kupambana kushare cv’s na kuamini kua wakati wa mungu ni wakati sahihi ndugu zangu asikudanganye mtu AJIRA ZIPO amini tu na itakua inshallah.
NAWASILISHA