Ajira zipo, Mrejesho wa jinsi nilivyopata ajira kupitia jukwaa hili

Ajira zipo, Mrejesho wa jinsi nilivyopata ajira kupitia jukwaa hili

JF ina watu,
Nakumbuka ilikua 2020 nimesimama chuo niko mtaani sielewi... humu JF nikakutana na post ya mtu kulalamika mausala ya ajira halafu katika comments nikakutana na comment ya mkuu Mjusilizard anamuuliza kama anaweza kuandika makala za michezo amtafute, mi nikamrukia jamaa kumuomba kama atahitaji mtu mwingine mi niko tayari, Mjusilizard akanambia yule mshkaji hajamcheki hivyo kama naweza kufanya tuingie mzigoni.

Nilianza kazi (na sikuwa najua chochote yani mana nilichokua nafanya nacopy vitu sehemu mbalimbali napaste sehemu namtumia, sasa hapo lazima ukute fonts tofauti tofauti kwenye document moja hapo mi sielewi hata kama zipo tofauti basi angalau nibadilishe 😂 natuma hivyo hivyo jamaa akawa ananisahihisha na kunielekeza namna ya kufanya) nikaja kuiva, ikafika kipindi naandika makala zinachapishwa hadi Mwananchi huko.

Badae jamaa akaja kuniuliza kama naweza kuandika za niche ya travel/tourism, nikamwambia naweza kujaribu.. akanipa ABCs nikaanza kufanya na zile alikua ananilipa vizuri zaidi. Corona ilivyochanganya dili la tourism likafa na ile website wenye nayo wakaifunga.

Fast forward 2024 mwanzoni nilipigika sio poa, nina mbele sina nyuma 😂 nina watoto wawili kwa 2 different baby mommas, nina kidemu kinanipenda na kinanipa changamoto kweli niwe na hela nikiweke ndani... muda huo hata huko ndani sina mana baby mama wangu wa kwanza ninavoachana nae nilimuachia kila kitu chetu. Ikanibidi kumtafuta yule bosi wa ile website ya utalii (hapo kumbuka hanijui mana nilikua nafanya ghostwriting kwa bro Mjusilizard) kuna namna nilifikiria kwamba inawezekana ninachofanya sio sawa kwamba mtu anakufundisha kuvua samaki halafu unaenda kuvua kwenye his pond, tu nikakumbuka jamaa kwenye hatua za mwisho alitaka kuniachia lile dili moja kwa moja ye afocus na mambo mengine so nikafungua ki website uchwara nikawa naandika mambo mbalimbali kuhusu destinations hapa TZ, tovuti ilivokua kua nikaandika kuhusu hoteli ya yule bosi then nikam DM insta na link ya hiyo article... jamaa akaipenda na hilo likamfanya ashawishike kuirudisha ile tovuti tukaingia kazini mpaka leo.

Jamaa Mjusilizard tumeendelea kufanya dili za hapa na pale (japo dili la mwisho mambo yalienda south lakini I still got love for him, ni kwa sababu yake nilimuweka ndani mdada wangu na ninaweza kufanya biashara ninayoweza kuifikiria kuifanya.)

JF ina watu, Mungu atusaidie kutukutanisha nao.
Jf inatutoa watu wengi sana mkuu, watu wasikate tamaa
 
Back
Top Bottom