Akata tamaa baada ya kukosa kumpata mtoto

Joined
May 8, 2014
Posts
73
Reaction score
10
Nimatumaini yangu kuwa mko wazima ndani ya jukwaa. Ni furaha ya kila binadamu awe mwanamke au mwanaume kuwa na watoto lakini ikitokea kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu bila kufanikiwa kuwa na mtoto/watoto ndoa huwa chungu na haina amani wala furaha.

Ndugu zangu wana jukwaa, kuna rafiki yangu mmoja ameoa toka mwaka 2010 na hawakuweza kufanikiwa kumpata mtoto kwa zaidi ya miaka minne.

Walipoenda kupima majibu yao ilionesha hawakuwa ma tatizo la aina yeyote. Hawakukata tamaa waliendelea kumtafuta mtoto lakini bado mkewe hakuweza kushika ujauzito. Hii hali ikapelekea jamaa kuvunjika moyo na kuamua kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake bila mkewe kujua.

Mwanamke yule mwenye mahusiano nae aliweza kupata ujauzito, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba baada ya kumpatia mimba na mkewe nae akashika mimba, na kwa sasa wote wana ujauzito wa miezi 8.

Jamaa amechamganyikiwa hajui afanyaje, amwambie ukweli mkewe au laa! naombeni ushauri wenu kwa niaba yake maana ameniomba nimshauri.
 
Si useme tu ndo wewe.. any way watakushauri tu wazoefu
 
subiri wajifungue kwanza maana kwa umri huo wa ujauzito ukimwambia mkeo unaweza ukatafuta matatizo mengine ukajuta.
 
dah mechi za ugenini ni noumer

ujue nini usimwambie mkeo

endelea tu kutoa matumizi mpaka mtoto afikie umri flani hv ndo umlete mtoto home kwako umwambie huyu ni mtoto wako full stop hakuna maswali
 
huyo naye alikuwa na haraka mno miaka 4 tu anakata tamaa? asubiri wajifungue afu baadae awe wazi tu kwa mkewe nina rafiki yangu ameoa since 2005 hawajapata mtoto wanajipa moyo watapata tu
 
Hivi watu wakioana ni lazima wapate watoto?
 
Asichanganyikiwe bali atoe muda ukweli utakuwa wazi. Inawezekana kabisa amesingiziwa kotekote. Yaani mke ake naye alijaribu nje akashika ujauzito na huko alikochepuka kujaribisha amesingiziwa tu na siyo mhusika wa hiyo mimba ya mchepuko.
 
dah mechi za ugenini ni noumerujue nini usimwambie mkeoendelea tu kutoa matumizi mpaka mtoto afikie umri flani hv ndo umlete mtoto home kwako umwambie huyu ni mtoto wako full stop hakuna maswali
Wanaume wote wangekuwa kama wewe mie ningebaki single mother stress za nini?! Eti kirahisi tu umlete bila maswali thubutu!!!!! Ungekula ulikopeleka mboga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…