Elifuraha Longu
Member
- May 8, 2014
- 73
- 10
Nimatumaini yangu kuwa mko wazima ndani ya jukwaa. Ni furaha ya kila binadamu awe mwanamke au mwanaume kuwa na watoto lakini ikitokea kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu bila kufanikiwa kuwa na mtoto/watoto ndoa huwa chungu na haina amani wala furaha.
Ndugu zangu wana jukwaa, kuna rafiki yangu mmoja ameoa toka mwaka 2010 na hawakuweza kufanikiwa kumpata mtoto kwa zaidi ya miaka minne.
Walipoenda kupima majibu yao ilionesha hawakuwa ma tatizo la aina yeyote. Hawakukata tamaa waliendelea kumtafuta mtoto lakini bado mkewe hakuweza kushika ujauzito. Hii hali ikapelekea jamaa kuvunjika moyo na kuamua kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake bila mkewe kujua.
Mwanamke yule mwenye mahusiano nae aliweza kupata ujauzito, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba baada ya kumpatia mimba na mkewe nae akashika mimba, na kwa sasa wote wana ujauzito wa miezi 8.
Jamaa amechamganyikiwa hajui afanyaje, amwambie ukweli mkewe au laa! naombeni ushauri wenu kwa niaba yake maana ameniomba nimshauri.