Akata tamaa baada ya kukosa kumpata mtoto

Akata tamaa baada ya kukosa kumpata mtoto

Stress is when your wife is pregnant.
Tension is when your girlfriend is pregnant.
And Panic is when both are pregnant.

si kazi ya uumbaji jamani kwani ywf akiwa pregnant ni stress au sijakuelewa vizuri
 
Asubiri ajifungue amwambie, af ajifunze kuwa mvumilivu.
 
watoto ni matunda ya ndoa

Mimi ninavyofahamu ni kwamba ndoa ni darasa la upendo.

Yaani upendo huja kwanza kabla ya mambo mengine yoyote.

Hivi hujaona kuwa watoto huzaliwa hata na watu wasio wanandoa?

Je, hao watoto ni matunda ya nini? Hawastahili kuitwa watoto?
 
Nakubaliana nawe Mkuu, lakini kwa ndoa zetu za kiafrika inapotokea mke na mume hawakupata baraka hizo za Muumba wetu kupata watoto, basi wazazi, ndugu, jamaa na marafiki huanza minong'ono ya pembeni ambayo baadaye inakuwa si minong'ono tena na kuweza kuwaathiri wanandoa hata kuharibu ndoa yao.

Mkuu binafsi naamini kuwa na watoto si jambo la ulazima isipokuwa ni baraka tu toka kwa Muumba...
 
Ndivyo inavyojulikana.....tena wanakuuliza vipi ndoa bado haijajibu.....

Mzima lakini jirani.....

Wanajua hivyo ni kwa vile wameamua kuamini hivyo...

Nijuavyo mimi ni kwamba sheria ya kwanza ya ndoa ni upendo...

Na kama ujuavyo sifa za upendo kuwa huwa haujivuni, huangalii ubaya n.k
 
......kha?!....
Amwambie nini sasa mkewe?!

Alipoenda "kuchepuka" alimwambia? Hapana,....then mwache apige kimya huku akisubiria matokeo.

BTW, wenye hizo mimba wamejikalia kimya, yeye kihere here cha nini sasa?!

Nimatumaini yangu kuwa mko wazima ndani ya jukwaa la MMU.
Ni furaha ya kila binadamu awe mwanamke au mwanaume kuwa na watoto lakini ikitokea kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu bila kufanikiwa kuwa na mtoto/watoto ndoa huwa chungu na haina amani wala furaha.
Ndugu zangu wana jukwaa la MMU, kuna rafiki yangu mmoja ameoa toka mwaka 2010 na hawakuweza kufanikiwa kumpata mtoto kwa zaidi ya miaka minne. Walipoenda kupima majibu yao ilionesha hawakuwa ma tatizo la aina yeyote. Hawakukata tamaa waliendelea kumtafuta mtoto lakini bado mkewe hakuweza kushika ujauzito. Hii hali ikapelekea jamaa kuvunjika moyo na kuamua kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake bila mkewe kujua.
Mwanamke yule mwenye mahusiano nae aliweza kupata ujauzito, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba baada ya kumpatia mimba na mkewe nae akashika mimba, na kwa sasa wote wana ujauzito wa miezi 8. Jamaa amechamganyikiwa hajui afanyaje, amwambie ukweli mkewe au laa! naombeni ushauri wenu kwa niaba yake maana ameniomba nimshauri.




#MosKwito !
 
Mkuu naomba unifafanulie huo ulazima unatokea wapi? Yaani ni nini kiini cha huo ulazima...

Ni mazoea tu na mind set tuliyojiwekea wenyewe waafrika mkuu........

Children are the reward of life. ~ African proverb
 
nimatumaini yangu kuwa mko wazima ndani ya jukwaa. Ni furaha ya kila binadamu awe mwanamke au mwanaume kuwa na watoto lakini ikitokea kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu bila kufanikiwa kuwa na mtoto/watoto ndoa huwa chungu na haina amani wala furaha.

Ndugu zangu wana jukwaa, kuna rafiki yangu mmoja ameoa toka mwaka 2010 na hawakuweza kufanikiwa kumpata mtoto kwa zaidi ya miaka minne.

Walipoenda kupima majibu yao ilionesha hawakuwa ma tatizo la aina yeyote. Hawakukata tamaa waliendelea kumtafuta mtoto lakini bado mkewe hakuweza kushika ujauzito. Hii hali ikapelekea jamaa kuvunjika moyo na kuamua kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake bila mkewe kujua.

Mwanamke yule mwenye mahusiano nae aliweza kupata ujauzito, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba baada ya kumpatia mimba na mkewe nae akashika mimba, na kwa sasa wote wana ujauzito wa miezi 8.

Jamaa amechamganyikiwa hajui afanyaje, amwambie ukweli mkewe au laa! Naombeni ushauri wenu kwa niaba yake maana ameniomba nimshauri.
bila kujua mungu alikupa mtihani alitaka apime imani yako je utaendelea kumuamini?yaan ww miaka mi4 unalalama umechelewa kupata mtoto?ss umekengeuka na mungu kakumaliza kakuonesha kuwa mkeo sio tasa anazaa sasa kubali kuvunja ndoa kwa upumbavu wako,jipe moyo ila umeharibu dira yako ya uaminifu kwa waifu wako kubali kuchapiwa na ww ,
 
asa si nimesha mwambia ni mtoto wangu what else do you need to know ? mama wa huyo mtoto niliyemzalisha ama! wanawake sijui kwanini tunakuwaga na roho mbaya ishatokea mtoto huyo hapo the point ni kufocus whats next to be done kuhusu ishu muhimu za shule na mengineyo I learned this from my mother tulikuwa mimi ,dadangu na kakangu na mdogo wangu dingi enzi hizo niko darasa la tatu dingi aliwaleta kaka zangu wengine watatu akamwambia maza sikia hawa ni watoto wangu full stop , tumeishi nao vizuri wala hakukuwa na cha mama wa kambo wala nn na maisha yaliendelea tu kwani kuishi na huyo mtoto malaika wa Mungu kutakugharimu gunia za mchele kwa siku !the point isn't why it happened but whats next to be done
Pesa sio tatizo kwamba eti atakula gunia Mia hapana Sema nahitaji maelezo ya kina afu mambo hayo pia yanahitaji hekima ya mwanamke sio kila mtu anaweza kuishi na mtoto Wa nje!
 
Nakubaliana nawe Mkuu, lakini kwa ndoa zetu za kiafrika inapotokea mke na mume hawakupata baraka hizo za Muumba wetu kupata watoto, basi wazazi, ndugu, jamaa na marafiki huanza minong'ono ya pembeni ambayo baadaye inakuwa si minong'ono tena na kuweza kuwaathiri wanandoa hata kuharibu ndoa yao.

minong'ono yenyewe "mwanamke gani huyu anatujazia choo tu" ukute jamaa hasimamii shoo vizuri
 
huyo naye alikuwa na haraka mno miaka 4 tu anakata tamaa? asubiri wajifungue afu baadae awe wazi tu kwa mkewe nina rafiki yangu ameoa since 2005 hawajapata mtoto wanajipa moyo watapata tu

Wakati mwingine inabidi ufanye hivyo hasa kama mkeo anatumia tatizo hilo kuvunjia heshima, yaani ni msumbufu!
 
Back
Top Bottom