Akaunti ya Benki ya mtu aliyefariki

Kumbe inawezekana.... Leo mhudumu pale mahakamani anasema eti ni lazima ifungwe
Yuko sahihi...inafungwa na pesa inakua tranferred to BOT..kwa maelekezo toka mahakama,km kuna pesa za biashara zitakuja through that account,either zitarudishwa zilipotoka or bank itazizuia na kuwapata taarifa..ambapo idhini tena ya mahama itahitajika.
 
Asante sana maelezo yako yanaeleweka.
Na je kama baadhi ya wanufaika kama wazazi ambao ni wazee wa kijijini hawana account bank??
Ni lazima uwafungulie account, siku hizi kufunguwa account ni dakija tano tu.

Hizo pesa hapewi mtu yeyote mkononi, wanufaika wote wanaingiziwa kwenye account.

Subiri mkipata fomu za mgawanyo wa pesa mahakamani, zile fomu sasa wafuate kijijini wafungulie account then utawajizia fomu watasaini halafu watakaa wanasubili tu mzigo wao usome kwenye account.

Wakati wa shauri utamueleza uhalisia hakimu kwamba kuna wazee afya haziwaruhusu kufika mahakamani kwahiyo mnawawakilisha nyinyi chini ya hati ya kiapo.

Halafu kwenye process nilisahau mkishafunguwa mirathi inabidi muende kuitangaza kwenye gazeti la uhuru na lile gazeti likitoka mkate kile kipande cha tangazo unakileta mahakamani kinakaa kwenye file.
 
Ni gazeti la uhuru au lolote la serikali?
 
Sawa ngoja niwaite wafungue account
Siyo lazima kuwaita, unaweza ukasubiri stage mtakayopewa fomu za kujaza mgao wa pesa ukaenda wewe na fomu ukawafungulia account ukawasainisha fomu unaondoka na copy tu za kadi zao za bank, huna haja ya kuwasumbuwa.

Ukipata mtu wa kukupa muongozo stage by stage ni mambo rahisi tu kama kwenye familia mko vizuri hakuna mnachogombania.

Unaweza kumaliza huu mchakato wote si kwa zaidi ya miezi mitatu tu pesa tayari zitakuwa kwenye account zenu.
 
Asante kwa elimu mkuu ila hiyo kaa kimya yako imekaa kishari sana. Sio ugomvi ndugu.
 
Mideko upo sahihi na huu ndiyo utaratibu lakini sio kuhamishiwa kwenye account ya mahakama
 
Huwezi kuanzia benk unaenda kwanza na hizo documents mahakamani na baada ya mahakama kukupitisha kama msimamizi wa mirathi ndio wanakupa barua ya utambulisho unaenda nayo bank
Shukran pia kwa elimu
 
Ndiyo inawezekana...

Mleta mada natumae umepata muongozo...
 
Financial Institutions zinafaidikaa sana kwenye hili suala. Watu wanaficha pesa kwenye mabenki bila kuwataarifu family zao, mzee kifo akifanya yake, hakuna anaejua pesa ipo wapi na ni kiwango gani!

Andika mirathi tafadhali, alaaa!
 
Ni gazeti la uhuru mkuu, weka siasa pembeni, ccm ni jinamizi ambalo haliwezi kuwaachia Watanzania leo au kesho.
Haulazimiki kuwa gazeti ka Uhuru peke yake,mimi mwaka juzi nilipeleka katika gazeti la Mwananchi ofisi zao zipo pale Jmall building,gazeti lolote lenye wigo mpana kwenye usambazaji
 
Dr matola naomba msaada wako nna changamoto kama hii naomba nitafute 0685280541
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…