Kuna members wamekupa maelezo sahihi ila ngoja nikunyooshee kidogo.
Je wewe ni mnufaika wa hiyo mirathi, kama ndio je hizo pending transaction zinatalajiwa kuingizwa lini kwenye hiyo account?
Kama ni hivi karibuni subilini msifunguwe mirathi kwanza pesa iingizwe.
Pesa ikishaingizwa mnafunguwa mirathi ambapo utaratibu ni kwenda mahakamani na mukhtasari wa kikao cha familia ambao mmeteuwa msimamizi wa mirathi, mukhutasari ugongwe muhuri wa serikali ya mtaa, ni vizuri mkiandika kwa mkono msichape tafuteni mwanafamilia mwenye muandiko mzuri atawaandikia.
Mkishafunguwa mirathi mahakamani kama hakuna malumbano yoyote ya kifamilia kugombea chochote shauri linapelekwa faster na msimamizi wa Mirathi anateuliwa na mahakama na anapewa barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi.
Sasa hapo ndipo mahakama itaandika barua kwenda bank husika kufunga account ya/za marehemu na kuleta hesabu ya pesa yote kwenye account ya mahakama, hii barua anapeleka msimamizi wa mirathi.
Baada ya hesabu kupokelewa kwenye account ya mahakama, msimamizi wa mirathi atapewa fomu ya idadi ya wanufaika/ warithi ajaze mgawanyo wa pesa yote ya marehemu kwa wanufaika bila kuzidisha hesabu wala kupunguza kwa kile kilichopo kwenye account.
Mkishakamilisha kujaza hizo form na kuzirudisha mahakamani zikiwemo copy za card zenu za bank basi kifuatacho ni kusubiri kwa muda kama wa mwezi mmoja utasikia msg kwenye simu muhamala umeshasoma kwenye account zenu simple as that.
Kama kuna vitu sensitive unaona vinakusumbuwa nicheck private nitakupa muongozo wote, hakuna kitu kinaniuma kama mtu anafariki halafu pesa zake zinapotea kwa sababu ya kukosa backup tu na baadaye familia inaishi kwa dhiki wakati marehemu aliwaandalia maisha na future nzuri.