x
Kabla hatujamlaumu Riz1, je wewe mwenyewe unayo angalau agency ya kutoa vijana wasio na kazi sehemu moja kwenda nyingine hata ndani ya TZ kwa kazi kama vile shamba boy, housemaids, kuuza maduka, bars n.k?! Nimekuuliza kwa sababu kazi nyingi za aina hiyo Kenya sio kwamba zinatafutwa na serikali bali na agencies na ndo maana kuna Wakenya wengi sana Arabuni kabla ya huyo Mutua!
Unaonekana una uwezo mdogo wa kufikiri, Tanzania tuna balozi ngapi zipo Tanzania hapa za Nchi nyingi? Waziri anashindwa kwenda kuuliza huko kwenu Kuna fursa gani japo vijana kadhaa waende wakapate Kazi ? kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira kama Nchi imeshindwa kutengeneza mazingira mazuri ya kuwapa Ajira walio na vigezo Kuna ubaya gani wakaenda huko nje ili wawekeze Tanzania.. Tena hakuna kitu kizuri kama serikalini ikawa ndio imekudhamini sababu sio rahisi kudhulumiwa maslahi Yako
Sasa mnataka vijana wabaki mtaani wanabanana mnafurahia mnappita Kazi zenye uhitaji watu 500 wanakuja watu 9000 kwenye usaili.
Ubinafsi Roho za Chuki kuwa na vigezo wasio na Upeo Viongozi wenye uwezo mdogo kabisa tunasikitika Sana wanasiasa wenye uwezo mdogo ndio wanapewa dhamana ya kuongoza Raia
Tuna balozi nyingi hapa Germany, finland, U.K , UAE wao wameshindwa vipi? Kuna balozi wapo mtandaoni kuandika sijui "quotes" waonekane wanabusara ujinga mtupu .
.
Tukiwa Nje ya Nchi unakutana na wakenya na nchi zingine unajiuliza Tanzania Tatizo nini?
Mtasingizia Lugha huo ni Uongo nimetembea Nchi nyingi Lugha ya kiingereza ni baadhi ya maeneo tu wengi wao Lugha hawajui Sana maana inafundishika na Kuna maeneo mengine wanatumia wengi wao waliopo hapo Poland, German , Luxembourg, Switzerland, n.k English siyo lugha ya kwanza Kuzungumza
Kaa fikiria angalia viongozi wenye hiyo dhamana wanauwezo kweli? Wao furaha yao kukaa kwenye hizo gari kula posho kununua magoli na kusuburia uchaguzi ufike waende wakagalegali kwenye mchanga kuomba Kura vijana ambao ni 23-35 wengi hawana Ajira wengi wao wanaamua kujiajiri katika bet na kushabikia simba na yanga kufanya parade
Vijana nawashauri pia muwe mnamoyo wa kusaka fursa Nje zenye ujuzi na zisizo na ujuzi vijana kadhaa nimekutana nao Netherlands, Germany, Poland USA lakini sio wengi kama wenzetu.. tumieni mitandao vizuri