- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hili sakata la dola linanivuruga sana, ukifuatia kulikuwa na taarifa mtandaoni kuwa Tanzania kuna uhaba wa dola Za kimarekani.
Sasa naona tena kuna taarifa inazagaa mtandaoni kuwa BoT akiba hiyo imekauka kabisa, na si dola pekee sasa hadi shilingi ya Tanzania nayo imekauka.
Kuna ukweli hapa wakuu?
---
Sasa naona tena kuna taarifa inazagaa mtandaoni kuwa BoT akiba hiyo imekauka kabisa, na si dola pekee sasa hadi shilingi ya Tanzania nayo imekauka.
Kuna ukweli hapa wakuu?
---
- Tunachokijua
- Benki Kuu ya Tanzania ni benki ya kitaifa inayosimamia masuala ya kibenki na kifedha nchini Tanzania.
Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania
- Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania
- Kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha
- Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini.
- Kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
- Benki ya Serikali
- Benki ya Mabenki; na
- Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Ukweli ni upi juu ya kukauka kwa dola ya kimarekai pamoja na shilingi ya Tanzania Kenki Kuu
Tarehe 16, 08, 2023 Tanzania leaks walichapisha habari kupitia mtandao wa Twitter kuwa wana taarifa za uhakika kuwa Benki ya Tanzania imekaukiwa dola na shilingi.
Benki Kuu ya Tanzania tarehe 18, 08, 2023 imekanusha kupitia mtandao wa twitter juu ya madai kuwa imekaukiwa na dola kwa kuandika kuwa huo ni uongo na unapaswa kupuuzwa.
Julai 17 2023, Beni Kuu ya Tanzania kupia kwa Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba, ilikiri kuwepo kwa upungufu wa Dola za Kimarekani huku ikiwatoa hofu watanzania kuwa uhaba huo haujafikia kiasi cha kuleta hofu.
JamiiForums, imethibitisha kuwa taarifa ya kukauka kwa dola za Kimarekani katika benki Kuu ya Tanzania si ya kweli, na kwamba kilichopo nchini ni upungufu(uhaba) wa Dola na si kukauka kabisa.