Akikuonya uachane na mkewe, acha usilazimishe yasikukute kama haya

Akikuonya uachane na mkewe, acha usilazimishe yasikukute kama haya

Wewe unaonekana ni mchepukaji tu kama huyo aliyeuliwa (ndege wafananao huruka pamoja).Nasema hivi, mwenye mke yupo sahihi,tena ilipasa aondoke kabisa na mizoga yao akapike nyama.NA WEWE ENDELEA KUCHEPUKA NA WAKE ZA WATU,DAWA YAKO IPO JIKONI INACHEMKA.
[emoji3]
 
Wabishi watakupinga na hili wakidai umejitungia, Watu hatufanani na si kila Mtu ana uwezo wa kuvumilia yanayomsibu ndiyomaana wengine huua na hujinyonga.
Ishu kama hii iliwai kutokea ukonga maeneo ya moshibar pale relin mjeda alikuwa na .mchepuko wake anahuudumia kwa kila kitu akaja kusikia mchupuko wake unamegwa na kijana muuza mahindi ya kuchoma pemben ya balabala mjeda akatoa onyo lakin kijana hakusikia siku ya siku mjeda akachukua gari yake adi mbele ya muuza mahindi gar ikiwa inaangaliza usawa wa muuza mahindi alifanya nini sijui au ndo mbinu za jeshi ile gar ikawa kama ilonasa vijana tulokulia uswahilin tunasema Inaslip akaita vijana waje waisukume maana imenasa kumbuka gar inasukumwa kwa mbele alipo muuza mahindi vijana ile kuisukuma tu jamaa kachochea mafuta kibat kagonga jiko muuza mahindi adi maind yenyewe mungu alikua upande wake muuza mahindi kapona ila alichokuja kumfanyia bola muuza mahindi angekufa kwa ajal ya ile gari mhhh aligeuzwa nyama za mishkaki

Nb.wanaume ikifika stej adi mwanaume mwenzio kufunga safar kuja kukupa onyo Msikilize awe mke au mchupuko achana nae...
 
Ni siku tatu sasa tumemaliza mazishi ya watu wawili; Mwanamke na Mwanaume na wote walikufa siku moja kwa tofauti ya masaa tu.

Maneno mengi yalisemwa ila kubwa na lililoteka hisia za wengi ni hili....

Mwanamke aliekufa ni mke wa mtu na mwanaume aliekufa alikuwa ni mseja yani kamtaliki mkewe hivyo akawa na mahusiano na mke wa mwenzake.

Mwenye mke alijua mahusiano yao, akamuonya mkewe ila mwanamke hakusikia.
Mwenye mke akaona ni vyema amfuate mume mwenzie na kumuonya ila mwanaume akampiga mwenye mke na kwa nguvu ya pesa akamweka kolokoloni.

Kesi ikakosa nguvu jamaa akatoka na kukuta bado mkewe analiwa kama kawaida.

Hakuwabugudhi akawaacha.

Mwenye mke nae alikuwa na marafikk wenye magari, jumatano,akaazima gari la best yake na alipewa.

Hakuna aliejua lengo ni nini.

Mkewe nae akaaga nyumbani, akapakiwa kwenye gari la mchepuko na kwenda lodge kisha mchepuko akaita dereva na kurudisha gari yeye akabaki na pikipiki aliokuja nayo dereva wake,wakapigana miti tani yao, jioni wakapakiana kwenye pikipiki na kuanza kurudi walipofika maeneo ya 4way(Dodoma),wakapata ajali ya kugongwa na gari vibaya sana yani mke na mchepuko wake.

Mchepuko alikufa palepale na mwanamke alifia njiani akipelekwa hospital ya mkoa(Genero).

Aliegonga ndie mwenye mke akiwa na gari la kuazima.

Sasa mjuavyo kesi ya kugonga na kuua ni kama hamna kesi hivi(madereva wanafahamu).

Tumezika huku mabaharia tukiwa tumepata funzo kubwa sana.

Usijifariji kwamba maziwa unayo geto, vidosho ni wengi anaegarimikia mke muache na mkewe
Au ndio hawa tumewazika kijiji Lugala
 
Mwanaume mwenye tabia ya kutembea na wake za watu siku zote anajiamini na kwa jinsi alivyofanikiwa kukuzunguka haamini kama siku moja anaweza fumaniwa...
 
Basi labda tuko tofauti sana mkuu.
Mimi binafsi wivu ninao lakini napingana sana na wanaosema wanaweza kuuwa kisa mkee.

Huwenda tumeumbwa tofautiii,mke hawezi kuniuma kiasi nimtoe uhai.

Kama yeye ndo furaha yangu,nikimuua nitaipata wapi furaha?
Kama nakubali kwamba yeye ni furaha yangu basi vipi nimuue?
Kama sio furaha yangu sasa huo wivu unatoka wapi?
Au ni kukomoa na kulipa kisasi?

Hakuna mantiki juu ya hilo,ni roho ya kipuuzi na kikatili tu ambayo mtu imemjaa kutokana eidha na mazingira alozaliwa au namna alivyojikuza...

Alafu kuhusu mahari ya kuolea labda nikudokeze jambo moja kwambaa.... Haina maaana ya kwamba kutoa mahari kubwa ndo unampenda sana mwanamke,na wala haina maana kutoa mahari ndogo haumpendi mwanamke.

Kama ni hivyo basi jua kwamba uliyemuoa kwa mahari kubwa hakupendi kwa nini ujuee ? Kwa sababu kama anakupenda mahari kubwa ya nini ?
Kakupenda wewe ama kazipenda pesa zako ?

Hivyo kama umeoa kwa mahari kubwa basi tafsiri yake(kwa mujibu wa kauli yako)ni kuwa huyo mke hakupendi na kama hakupendi kwa nini asichepuke kutafuta anaowapenda?

Kwa sababu si ndo tunasema mwanamke anayekupenda wewe hajali pesa zako wala hakuombi ombi pesa,sasa iweje mwanamke anayekupenda atake mahari nyingi ?
Basi kwa huo msemo wako jua kwamba akitaka mahari kubwa hakupendi na hapo zinduka wewe sasa uone kwamba kama anataka mahari kubwa =hanipendi.na kama hanipendi basi nikimuoa atachepuka kuwatafuta anaowapenda.

Ebu kuwa siriaz mkuu haya mambo siriaz usiingize mzaha kabisaa

Huyo asisingizie wivu kabisa.
Yameisha siongezi neno
 
Ndo mana yesu akafa msalabani kumbe?

Na pale mnaposema kwamba binadamu asimhukumu binadamu mwenzie mna maana gani?

Au pale mnapotoa kisa cha mzinifu akawa anataka kupigwa kisha akainuka mtu akasema "ambae ni msafi kabisa hana dhambi basi ampige huyo mzinifu" alafu hakuinuka mtu je hivyo visa vina maana gani?
Mshahara wa dhambi ni mauti "Bible verses"
 
Nimeoa mkuu lakini mke wangu akichepuka siwezi kufanya huo ujinga hata siku moja.

Mtu umeshamuacha tayari alafu unaendelea kumfaatilia mkuu?
Kama huyo mke alikuwa anabakwa sawa lakini kama anafanya kwa ridhaa yake naona jamaa alipanick sana
Ngoja nije nimchukue mkeo halafu nikutumie na video nzima,.
 
Yani kabla ya tukio uwe na matokeo.
Mimi matokeo nishayapanga kabla ya tukio kwamba naacha niumie kwa muda nitapoa.
Ngoja nije nimchukue mkeo halafu nikutumie na video nzima,.
 
Tahadhari muhimu sana mkuu.
Kuchepuka sio issue
Ukiona mtu anakukataza kwamba achana na mke wangu Jua ashakumaliza ananawa tu mikono kama Pilato ili damu yako iwe juu yako
 
Sasa ww hapo kipi si cha kweli stori au kesi?
Walikuja kupima ajali ni trafiki, na kesi ni ajali wala sio mauaji na sheria zinafuatwa kulingana na tukio lilivyo.

Hiyo umesema wewe kwamba kaua kwa kukusudia ila sheria haimuoni kama ni muuaji kwa sababu waliogongwa walikuwa kwenye chombo cha moto.

Hivyo nimeandika nikiwa najua nilichoandika ndugu, sheria haipo kwa mawazo binafsi. Na hata dhamana alipewa na anasubiri kulipa faini mahakamani.

Afu nikwambie kitu kwenye masuala ya ndoa sheria ipo wazi kabisa yani hata kama angeua kwa mkono, kwa sababu kaua wote kesi huwa ni ndogo mana inachuliwa aliua bila kukusudia ila aliendeshwa na hasira, lakini akiua mmoja akaacha mmoja inachukuliwa aliua kwa kukusudia (endapo aliwakuta yani aliwafumania) ila akifanya kwa kuwakuta mtaani sheria inamtambua kama muuaji kama wauaji wengine.

Wewe ndo unataka kupindisha sheria kwa mawazo binafsi
Defense ya provocation inaweza kuwa applicable kama kitendo kitakuwa kimefanyika muda ule ule ambao aliwafumania.

Mazingira hayo yanaonesha kuwa kulikua na muda mrefu wa kufanya maamuzi mengine,(time for cooling) kwakuwa aliwafuata kwa muda mrefu na kuwagonga.
 
Ni siku tatu sasa tumemaliza mazishi ya watu wawili; Mwanamke na Mwanaume na wote walikufa siku moja kwa tofauti ya masaa tu.

Maneno mengi yalisemwa ila kubwa na lililoteka hisia za wengi ni hili....

Mwanamke aliekufa ni mke wa mtu na mwanaume aliekufa alikuwa ni mseja yani kamtaliki mkewe hivyo akawa na mahusiano na mke wa mwenzake.

Mwenye mke alijua mahusiano yao, akamuonya mkewe ila mwanamke hakusikia.
Mwenye mke akaona ni vyema amfuate mume mwenzie na kumuonya ila mwanaume akampiga mwenye mke na kwa nguvu ya pesa akamweka kolokoloni.

Kesi ikakosa nguvu jamaa akatoka na kukuta bado mkewe analiwa kama kawaida.

Hakuwabugudhi akawaacha.

Mwenye mke nae alikuwa na marafikk wenye magari, jumatano,akaazima gari la best yake na alipewa.

Hakuna aliejua lengo ni nini.

Mkewe nae akaaga nyumbani, akapakiwa kwenye gari la mchepuko na kwenda lodge kisha mchepuko akaita dereva na kurudisha gari yeye akabaki na pikipiki aliokuja nayo dereva wake,wakapigana miti tani yao, jioni wakapakiana kwenye pikipiki na kuanza kurudi walipofika maeneo ya 4way(Dodoma),wakapata ajali ya kugongwa na gari vibaya sana yani mke na mchepuko wake.

Mchepuko alikufa palepale na mwanamke alifia njiani akipelekwa hospital ya mkoa(Genero).

Aliegonga ndie mwenye mke akiwa na gari la kuazima.

Sasa mjuavyo kesi ya kugonga na kuua ni kama hamna kesi hivi(madereva wanafahamu).

Tumezika huku mabaharia tukiwa tumepata funzo kubwa sana.

Usijifariji kwamba maziwa unayo geto, vidosho ni wengi anaegarimikia mke muache na mkewe
Umenikumbusha mbali sana mkuu... Road Traffic Act imewalinda mno madereva.
 
Wanaume kama huyo jamaa nawaonaga wapumbavu sana yaani.
Mke anauma lakini haujazaliwa nae tumbo moja.

Hivi hawajiulizi kwa nini wale tuliozaliwa nao tumbo moja ni haramu kuwaoa?
Kwa sababu ukimuoa dada yako ama shangazi yako alafu ukahisi kuna mtu anakuchukulia,wivu unakuwa spidi kali sana.

Tunawaoa wasiokuwa wa damu moja kwa moja yaanintunawaoa wale ambao damu hazijaingiliana sana kuepusha wivu wa kipumbavu kama huu wa kuua,mtu umekutana nae tu ukubwani unamuoa alafu unajifanya una wivu sana mpaka una muua ina maana wakati wote alikuwa anaishi kwa ajili yako mpaka sasa uone hafai kuishi?

Na kama mke ndio chanzo cha furaha yako ina maana unapomuua huoni kwamba utakosa furaha milele kwa kumuua?
Sasa ukishamuua nani atakupa furaha bali ndo utazidu huzuni ya kukosa furaha na huzuni ya kuua furaha yako.

Akikusaliti na ulishamuonya sana basi jua hakutaki,unachotakiwa kumhukumu ni kumwbia aendee kwa anayemchepukia.huo ndo uamuzi wa kiume japo utaumia lakini maumivu yana karibisha amani mbeleni.

Jamaa mpuuzi sana yani ila sawa.

Jamaa bwege sana yani kajipatia dhambi ya bure kwa jambo la kijinga sana.

Wanaume wenzanguu eee
"dont make a parmanent decision over a temporary circumstance"

N:B. Mke anauma
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom