Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Kampuni zinazojihusisha na nyanja ya akili mnemba (AI) hutoa madai mapana kuhusu uwezo wa zana zao kuchukua nafasi ya nguvu kazi ya binadamu.
Baadhi ya kazi zitaendeshwa kikamilifu na mifumo ya kiotomatiki, huku nyingine zikibadilishwa na kuboreshwa kwa kutumia akili mnemba.
Viongozi wa makampuni makubwa zaidi duniani wanawekeza mabilioni ya dola katika teknolojia hizi, huku wakijua kuwa matumizi ya zana hizo yanaweza kupunguza gharama za nguvu kazi.
Siku hizi, watendaji wa makampuni wanaambiwa kuwa "kudumisha idadi ileile ya wafanyakazi ni ishara ya mafanikio na tija," wakati huohuo wawekezaji wakihoji iwapo kazi zinapaswa kukabidhiwa kwa wafanyakazi wapya au kwa "mawakala wa akili mnemba" wafanyakazi wa kidijitali walioajiriwa kufanya kazi mahususi, ambapo baadhi yao wana uwezo hata wa kufanya kazi zinazohitaji utaalamu maalum.
Ikiwa hata nusu ya madai haya ni ya kweli, athari zake zitahisiwa na sisi sote, katika sekta mbalimbali za uchumi na katika taaluma zetu. Mabadiliko haya yanaweza kutokea mapema zaidi kuliko tunavyodhani.
Wanauchumi waliotunukiwa Tuzo ya Nobel hivi karibuni walionya kuwa dunia lazima "ichukue hatua sasa" ili kuhakikisha kuwa akili mnemba inaleta ustawi na kuboresha viwango vya maisha, badala ya kusababisha upotevu mkubwa wa ajira.
Mwezi uliopita wafanyabiashara jijini London walionya kuwa wanapata changamoto kupata ujuzi wanaohitaji huku akili mnemba ikileta mabadiliko makubwa katika soko la ajira.
Bado tuko katika hatua za mapema, lakini takwimu tayari zinaonyesha mwelekeo fulani wa kuvutia. Takwimu hizo zinaonyesha jinsi mifumo mbalimbali ya akili mnemba inavyoweza kufanya kazi ambazo hapo awali zilifanywa na binadamu