Akili mnemba (Artificial Inteligence) Waafrika tumezaliwa nayo sema basi tu elimu yetu tulishindwa kuiweka kwenye mfumo

Akili mnemba (Artificial Inteligence) Waafrika tumezaliwa nayo sema basi tu elimu yetu tulishindwa kuiweka kwenye mfumo

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2022
Posts
791
Reaction score
1,852
Akili mnemba (AI) siyo kitu kigeni saana!

Afrika kwa asili tumezaliwa nanuwezo mkubwa wa kuunda akili mnemba sema basi tu hajui kuendeleza au kuweka vitu vyetu katika mfumo.

Maana rasmi ya akili mnemba ni akili bandia!

Lakini ukiniuliza mimi fundi SAMICO nikueleze kwa kina hii akili bandia ni nini nitakujibu hivi.

Akili mnemba (AI) ni nguvu asilia inayokusaidia kufanya jambo ulitakalo kwa niaba yako!

Kwa lugha rahisi akili mnemba ni RAMLI YA KISAYANSI!

Je, hii ni teknolojia mpya?

Akili mnemba siyo teknolojia mpya bali imekuja na kifungashio cha kizungu!

Mimi niliyekulia kijijini hii teknolojia ya akili mnemba tuliitumia sana katika mambo mengi kwa mfano;

1. Nilipokuwa nachunga ng'ombe kijijini kuna mdudu jamii ya kumbikumbi ilikuwa ukitaka kumuuliza akuelekeze mahali malisho au maji yaliyo aliweza kukuonesha kwa ishara na ukiifuata unayakuta maji.

2. Kule kijijini wakulima badala ya kukaa shambani kulina ndege wasimalize mazao, nakumbuka nilikuwa nachukua makopo nayakata natengeneza kama muundo wa panga za feni halafu natega kwenye upepo nayaunganisha na fimbo, halafu kwa pembeni naweka madumu ya bati ya (zamani yaliitwa KORIE)

Vile upepo ukisukuma ile feni ndiyo fimbo inapiga kama goma ndege wanakimbia.. Hii nayo ni akili mnemba, ambayo ingeboreshwa na kuundiwa sanamu la.mtu na kuvishwa kofia huenda ingevutia sana kama (AI)

3. Zipo RAMLI kwa ajili ya mambo mengi sana hadi sasa zinazoweza kukupatia taarifa ili uweze kuamua au kughailisha jambo zote hizi ni AKILK MNEMBA!

Wakati wa kampeni viongozi wengi huanza kwanza kupiga RAMLI Haya ni moja ya matumizi ya akili mnemba.
4. Kupaa na ungo ni akili mnemba n.k

Kiufupi akili mnemba asili yake halisi ni nguvu ya ulimwengu ili kukusaidia kukuchagulia hatima yako!

Unapopasua nazi njia panda ni sawa na kuomba ile nguvu ya asili ikubadilishie chaguzi baada ya chaguo la awali kuwa gumu kwako.

Mambo kama hayo wataalam wanaingiza katika mfumo wa kisayansi na kuyarejesha afrika kwa majina ya kizungu (artificial intelligence)

Ukweli akili mnemba haitofautiani na RAMLI TU.

Kama Kuna ramli njema na ramli chonganishi hata kwenye akili mnemba zina faida na hasara!

Kwa mfano!

Unapotype kwenye keyboard huwa kuna maneno yanatokea kama mapendekezo (prediction text) maneno hayo ni kazi ya akili mnemba!

Sasa kwani hujawahinkuandika meseji nzuri watu unaowaheshimu kabisa HALAFU Prediction text (wakabadili maana ikaenda meseji ya matusi?
Mfano ..umeandika vizuri tu
MAMA NAOMBA KINU lakini yenyewe inapredict meseji inayosomeka hivi MAMA NAOMBA KU....
Kama mama siyo muelewa hii akili mnemba si inakuwa CHONGANISHI HAPO?

Afrika hata vitu vyetu tukiweka kwenye mfumo vinalipa
 
Back
Top Bottom