Mtagamenda
New Member
- Sep 2, 2021
- 1
- 2
AKILI NA UBUNIFU NI MTAJI MKUBWA KULIKO FEDHA
Habari za muda huu wanajamii forum leo katika jukwaa hili la story of change nina mada ninayoiwasilisha kwenu naombeni muipokee na ikaweze kubadilisha au kuongezea kile mlichonacho.Kwanza kabisa nianze na hadithi fupi kisha tuendelee na mada yetu tajwa hapo juu. Wadudu wengi wakati wa usiku huvutiwa na mwanga wa taa uwakao kutoka ndani ya nyumba, na hii hupelekea wengi wao kutamani kuingia ndani na hutumia njia mbalimbali ili kuhakikisha wanaingia. Na punde tu wanapofanikiwa kuingia ndani watapepea kila kona ya nyumba kwa furaha, kujiona ni washindi na kuhisi wameyapatia maisha na kuwadharau wale wenzao walioko nje kwenye giza walio shindwa kuingia ndani. Furaha yao itaendelea paka ifikapo asubuhi ndipo watakumbuka kuwa chakula chao cha kila siku kinapatikana nje na ule mwanga wa taa uliowavutia wakati wa usiku nje pia unapatikana tena ni mkubwa na mzuri kuliko ule wa ndani. Tatizo hua linaanzia hapa kwakua hawawezi tena kutoka nje kwasababu wamesahau waliingilia wapi hivyo wataendelea kuhangaika kutafuta njia ya kutoka huku matumbo yao yakiwa hayana kitu na hii hupelea kukosa chakula na mwisho kabisa kupoteza maisha.
Hii hadithi inatufundisha nini? Inatufundisha kua tamaa na kukosa uvumilivu wa giza la muda mfupi inatuponza watu wengi wengi kwakutaka tuishi maisha mazuri wakati hatuna mikakati dhabiti ya kutengeza mwanga katika familia zetu zenye giza. Na hii imepelekea watu wengi kujihusisha na njia zisizo sahihi katika kutafuta utajiri ambazo mwisho wake hua ni kupoteza maisha, kwenda jera, au kupata urahibu wa madawa ya kulevya pamoja na urahibu wa michezo ya kamari. Vijana wengi wamejikuta wakijihusisha na maswala ya ujambazi, utapeli,ujangiri, na uuzaji wa dawa za kulevya kwakua wanataka utajili wa haraka bila kua na mikakati thabiti ya kupambana na umasikini kwa njia zilizo sahihi.
Ni kweli kumekua na ongezeko kubwa la watu wasio na ajira nchini lakini hii isiwe sababu ya kuilalamikia serikari kwanini watu hawana ajira au kuwalalamikia wazazi kwanini hawaja tuwezesha mitaji. Huu sio muda wa kutafuta mchawi ni nani ila ni muda wa kutafakari nini kifanyike ili kupunguza tatizo hili katika jamii kwa sababu kumekua na ongezeko la vijana wanaoshinda vijiweni bila kazi yoyote wengine wanashinda sehemu za kubeti, wengine sehemu za kucheza play station na kushinda mitandaoni kwenye kurasa za watu maarufu, pia kumekua na ongezeko la wizi, utapeli wa mitandaoni, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya pamoja ongezeko la matangazo ya waganga wa kienyeji katika nguzo mitaani kwa lengo la kutapeli watu.
Nini kifanyike?
1. kwa ngazi ya watoto wa shuleni [/SIZE]
- Tujenge misingi ya kujitambua kwa watoto zetu: hili lianzie nyumbani kwa wazazi pamoja na shuleni kwakubadili mtaala unaotumika sasa na kuongeza masomo ya ujasiliamali kuanzia ngazi ya shule ya msingi pia somo la stadi za kazi litiliwe mkazo sababu ni moja ya somo ambalo litatusaidia katika kugundua kipaji cha mtoto na kukiendeleza ili badae kiweze kumtengenezea fedha.
- Pia kwa shuleni tuweke mashindano maalumu ya kiwilaya na kimikoa ya stadi za kazi na kwa wanafunzi watakao onesha ubunifu mkubwa katika kazi zao waweze kupewa motisha itakayo wasaidia kuendeleza vipaji vyao na hii pia itasaidia wale walio shindwa kujipanga kwa mwaka unaofata na naamini hili jambo likifanyika vizuri basi tutapata bidhaa na teknolojia mpya zilizogonduliwa nchini na badae zikaja kuinufaisha nchi na hawa watoto watajifunza kufikilia nje ya box na hawata tegemea tena kuajiriwa na tutakua tumetengeneza kizazi cha wachapa kazi.
- Pia wazazi tuwe mstari wa mbele katika kuvikuza vipaji vya watoto wetu na tusiwe watu wa kuwakatisha tamaa.
2. kwa vijana na watu wazima
Siku zote wanasema lichomozapo jua unaweza ukahisi halitozama tena. kwanini nimesema ivo? Iko ivi vijana wengi tuna amini siku zote tutakua ni vijana na hatuto zeka na tunasahau nguvu na maarifa tuliyo nayo leo iko siku vitaisha na tutakua hatuna uwezo tena wakutafuta na tutakua ni wazee ambao tunategemea watu wengine au kuishia kua ombaomba. Zifuatazo ni njia kama kijana ukizifata vizuri naamini tutaikwepa adha hiyo.
- Ubunifu: kwasasa kumekua na kundi kubwa la vijana waliothubutu kuanzisha biashara zao lakini wengi wao wanafeli kwa kukosa ubunifu wanafanya kazi kwa mazoea na kwakuiga wenzao wamefanya nini. Mfano kwa sasa kila kijana anataka auze nguo online kwa kufata mkumbo, kila kijana anataka afanye kazi kwenye ofisi kubwa au aanze biashara yenye mtaji mkubwa na kusahau kua matajiri walianzia mitaji midogo na ubunifu wao ndio ulifanya wakafanikiwa.
- Tutumie njia sahihi katika kutafuta kipato: siku zote ukitaka njia ya mkato basi mwisho wako hautakua mzuri kwasababu ukitaka utajiri kwa njia zisizo sahihi basi mwisho wasiku utajikuta umepoteza muda na kile kidogo ulichonacho. Baadhi ya vijana wamekua hawajishughulishi lakini wamekua wakitegema kubeti pamoja na michezo ya Kamari wakiamani watatiza ndoto zao. Wengine wamekua wakitafuta njia za mkato kutafuta utajiri na wamejikuta wamedondokea mikononi mwa polisi au kupoteza maisha na kudondokea mikononi mwa waganga wakienyeji feki wakiamini watawasaidia kupata utajiri.
- Uvumilivu: siku zote ukiona giza linazidi ujue kumekaribia kukucha hivyo usikubali giza la muda mfupi liharibu malengo yako. Vumilia atakama umekwama mala nyingi lakini amini iko siku shida zote zitapita na utayashinda majaribu na ndoto zako zitatimia
- Lugha nzuri kwa wateja wako: siku zote ndege hutumia mdomo wake kujenga kiota chake, kama hauta kua na lugha nzuri kwa wateja wako usitegemee miujiza kama kila siku wataendelea kuwa wateja wako. Tuache lugha za matusi au lugha za kuwakejeli wateja wetu na uwe na uwe na lugha nzuri itakayo imarisha mahusiano yetuna wateja wetu
- Tutumie vipaji vyetu: watu wengi tumekua na vipaji mbali mbali lakini shida ni kua hatuwezi kuvitumia vipaji vyetu kwa kujidharau wenyewe au kuamini hatuwezi kutimiza malengo kwa kutumia kipaji. Kama una kipaji cha kuimba basi hakikisha unaimba sana , kama ni uandishi basi andika sana , kama ni uchoraji basi chora sana na kama ni uchongaji basi chonga sana na kama unakipaji chochote hakikisha unakitumikia ipasavyo na iko siku kitakulipa.
Akili ni mtaji mkubwa kama utaitumia vizuri basi tegemea kufaidika na kila unachokifanya hata kama ni kidogo au umekosa fedha lakini akili ikitumika vizuri basi itakujengea msingi imara ambao itakusaidia katika kukuza biashara yako binafsi na kukuza pato la nchi.
Naombeni kura zenu wana jamii forum na mungu akawabariki wote.
Upvote
2