Akili Nyeusi: Siri za watu wanaocheza na mawazo na malengo yako

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
AKILI NYEUSI: SIRI ZA WATU WANAOCHEZA NA MAWAZO NA MALENGO YAKO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Shuleni ulifundishwa Masuala la Chemical reactions, ulifundishwa natural selection, ulifundishwa Frictions.
Maisha ni vita, au reactions simple unazoziona kimwili na kiroho na complex.

1. Kuna vita au reactions ambazo hazionekani kwa macho, vita ya akili ambapo mipango na malengi huka huko. Watu wanaokuzunguka wanaonekana wa kawaida, wanacheka, wanazungumza kwa upole. Lakini ndani yao kuna mbinu za siri zinazoweza kubadili maamuzi yako bila wewe kugundua.

Wengine sio Wachawi na wengine ni wachawi wanaokuonea wivu, lakini ili wakuathiri lazima wawe wataalamu wa saikolojia ya binadamu wanaojua jinsi ya kuingia kwenye akili yako na kuichezea kama mchezo Fulani hivi wa karata.

Hizi ndizo sifa za Akili nyeusi na wenye nazo. Akili za Giza na namna wanavyokuchezea shere...

1. Wanajua Kusoma Hisia Zako kwa Haraka
Wana uwezo wa kusoma tabia, sauti, na mwili wako kwa dakika chache. Wanajua ukiwa na hofu, tamaa, au udhaifu Fulani na hapo ndipo wanapoanzia kukudhibiti.

Sisi Watibeli tuna njia nyingi ya kudili na watu wa aina Hii. Ndio maana unatakiwa udhibiti mihemko yako, don't show your weaknesses, keep distance na watu. Usipende kuonyesha siri na uwezo wako hasa kama haunufaiki kiuchumi.

2. Wanatumia Maneno Kama Silaha.
Ulimi ni silaha kubwa kuliko risasi. Ulimi ndio njia pekee wanayotumia kukushinda.
Wanatumia lugha laini, maswali ya hila, na sentensi zinazokufanya ujisikie unawajibika au una deni. Polepole unajikuta unafanya maamuzi yao, si yako.
Maswali ya hila unayajua? Hii ni mada ya Siku nyingine. Adui zako uliowafanya matafiki au waliopo karibu yako maneno Yao ndio silaha ya kujua nini kinaendelea kwenye akili yako na mipango yako.
Mtu anakupa pole na kukutia moyo sio ili akusaidia bali kama nyenzo yake ya kukusanya data na kukuhujumu.

3. Wanacheza na Uaminifu Wako
MTU hawezi kukuchezea akili au moyo wako kabla hajatengeneza uaminifu. Hivyo Kwanza wanajenga ukaribu.wanakuwa wasikivu, wema, na wanaojifanya wanakuelewa. Hapo utaanza kuwaamini. Baada ya kukuaminisha, ndipo wanapoanza kukuathiri polepole wakirusha kete zao bila wewe kushtuka. Hapa ndipo wengi hunaswa bila kujua. Kanuni ya trust no one ipo kwaajili watu wako wakaribu sio Kwa strangers. Wengi wanakuambia sikuamini Kwa sababu sikujui. Wakati hutakiwi kumuamini mtu yeyote.
Sisi Watibeli sio rahisi kuumizwa kwa sababu hatuamini yeyote hata Mama zetu waliotuzaa.

4. Wanajua Hofu na Tamaa Zako.
Katika maisha yako usipende watu wajue vitu unavyovipenda, na vitu unavyovihofia. Na tamaa yako.

Kila binadamu ana vitu viwili vikubwa: anachokiogopa na anachokitamani. Watu wanachimba hapo. Wanaweza kukutisha kidogo au kukupa matumaini makubwa ili wakudhibiti. Wanakutisha wajue hofu yako. Wanakupa matumaini wajue tamaa yako iko wapi.

5. Hawajionyeshi Moja kwa Moja.
Niliwahi kusema Rafiki ni Adui aliyekaribu.
Tofauti na watu wabaya wa wazi, hawa wako kimya. Wanajificha kwenye urafiki, mahusiano, au hata kazi. Ndiyo maana ni hatari zaidi, hawatambuliki kirahisi. Labda uwe mtu WA kusoma patterns na kuunganisha dots ndogondogo.

Dunia ya leo siya kutumia nguvu tu, bali niya kutumia akili. Ukiwa hujui mbinu hizi, unaweza kuishi maisha ambayo si yako ukiongozwa na watu wengine bila ya wewe kujua. Kujitambua ni silaha yako ya kwanza. Ukijua jinsi akili yako inavyoweza kucheza, utakuwa huru zaidi kuliko wengi.

Hizo ni sehemu ya Dark games. Kufikia hapo zina la ziada.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Dogo big up sana kwa huu uzi yani ni bonge la elimu. Shukrani za dhati mtibeli.
 
Back
Top Bottom