- Dopamine
- Acetylcholine
- Endolphin
- GABA
- Oxytocon
- Serotonin
- Na zinginezo nyingi
MImi nitajikita kuizungumzia dopamine zaidi, Dopamine ni kemikali ya FURAHA,
Ukiwa unatafuta kitu au jambo flani ukilipata dopamine huzalishwa kwenye ciruit, mfano wewe ni shabiki wa ARSENAL na mechi inapigwa kati ya Arsenal na CHELSEA mpo kibandani au uwanjani mnacheki game, matarajio yako ni arsenal ishinde, Arsenal wakifunga goli ubongo wako (circuit inayohusika na mpira) inazalisha dopamine, hii kemikali inapozalishwa mwili wako unasisimka unajikuta unalipuka kwa furaha,
View attachment 1911179
Baada ya muda (dopamine) kemikali inayeyuka unarudi kawaida, hii ndio starehe ya watu wengi
Lakini pia ufanyaji wa tendo la ndoa wakati unapofika mshindo (kumwaga mbegu) ule utamu unao usikia ndio dopamine hapo inazalishwa kwenye ubongo na huwa inamwagwa nyingi sana sana sana, ikiisha unarudi kawaida mpaka ijitengeneze tena ubomgoni ndio usisimke ndio maana huwa unapumzika kwanza au kuuchapa usingizi
Watu wanapenda mademu sababu kuu ni utamu (dopamine)
Kuna njia za bandia na hatarishi za kuufanya ubongo wako uzalishe dopamine yaani ujisikie furaha kwa njia fake
Mfano uvutaji bangi, unywaji pombe, matumizi ya madawa ya kulevya n.k hivi vitu vinakemikali inayofanana na dopamine, hivyo basi huufanya ubongo upokee kiasi kingi zaidi cha dopamine, inafikia wakati ili ujisikie furaha utahitaji bangi au pombe nyingi zaidi sababu mzunguko ushavurugwa na bangi au pombe
Ndio addiction hutokea hivyo