Akili ya kitajiri

Akili ya kitajiri

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Ulishawahi kujiuliza, kwa nini ukienda dukani unaweza ukakuta kitu cha shilingi 50, 100, 200 n.k?

Je hivyo vitu vinatoka wapi, ni kiwandani au ni mtu anajitengenezea? Mfano kuna biskuti, pipi, jojo, nyembe, pulizo n.k

Ukipata jibu, utagundua vingine vinatoka viwandani, na hivyo viwanda vimewaajiri wasomi mbali mbali; na uuzwaji wa hivyo vitu kwa bei ndogo ndogo ya shilingi 50 n.k ndio vinavyowalipa wale waajiriwa wenye digrii zao mishahara.

Kwa mazingira hayo sasa; wewe mpambanaji unatakiwa uamke, anzisha na wewe bidhaa zako zionekane kwenye maduka mbali mbali; lasivyo utaajiriwa na kuwa mtumwa mpaka unakufa.

Unaweza kuanza kiutani utani tu; mfano unaweza kutafuta maduka 20 n.k, hao ukawa unawapelekea bidhaa yako, mfano karanga zilizokaangwa na kuwekwa kwenye pakti, baada ya siku mbili tatu unazungukia mauzo.

Bahati nzuri biashara kama hiyo haiitaji mtaji mkubwa; ni wewe kuweka aibu chini na kuchapa kazi.

Haya kazi kwenu wapambanaji.​
 
IMG-20240401-WA0308.jpg
 
Wengi huwa tunadharau vitu vidogo vidogo
Hakuna bolt au nati ya shilingi hamsini kwa muhindi.

Mfano aliowapa ndugu Equation x naomba nimuongezee. Issue sio big G au pipi.

Issue is the more you sell the more you get. Yaaani transaction yako iwe na muendelezo.

Faida katika duka la jumla la vinywaji kwa package ni 50-200 au 250 nadra sana kuvuka hapo.

Kreti la soda, box la Choco biscuits, kreti la bia, energy drinks au soft drinks ziingine. The more anauza ndio faida yake.
Ukiuza 250 * 1000 ni 250,000 hii hesabu unapata hata catton za maji kwa siku mbili tu.

The more you transact the more you profit
 
Back
Top Bottom