Akili sio kitu ni matokeo ya ubongo kufanya kazi ndio maana tuna namna tofauti ya "akili' kwasababu tuna namna tofauti ya ubongo wa kila mmoja wetu kufikiri.....
Huwezi kutafuta mahali ambapo utapata makazi ya matokeo yoyote yale.....
Mfano mwendo wa gari ni matokeo ya injini kufanya kazi,je unaweza kuuliza mahali ambapo mwendo unakaa ndani ya gari?
Mfano mwingine ni moshi wa gari,moshi ni matokeo ya mafuta kuchomwa,lakini unaona moshi unatoka kwenye gari,je unaweza kuuliza mahali ambapo moshi unakaa kwenye gari?
Nadhani hilo haliwezekani kabisa,akili kama ilivyo mwendo au moshi wa kwenye gari au kuni sio vitu ili vihitaji mahali pa kuwepo bali ni matokeo ya jambo fulani.....
Akili bni matokeo ya ubongo kufanya kazi hivyo huwezi kuuliza mahali inaokuwepo......