Akili za Chifu Mangungo wa Msovero

Akili za Chifu Mangungo wa Msovero

Hii nadhani ni Fikra Potofu kwa sisi Waafrika - Swali ni kwamba kwanini mikataba ya mjerumani na utamaduni wao uwe binding kwa Muafrika aliyepo huku kijijini....

Mbili unadhani Chief angekataa wangemwambia nini kwamba basi hatukufanyi kitu chukua ardhi yako au wangempiga kichapo na kuchukua cha kuchukua ?

In short mikataba hiyo ilikuwa kwa manufaa ya hao wanyonyaji / maharamia yaani mjerumani akiwa na ile karatasi ili aseme kwamba ni yetu na sio ya Muingereza wala muarabu (uliza maharamia wengine makaburu wa Afrika Kusini walifanywa nini na Muingereza wakati wanagombani Ardhi ya wenyeji wa pale)
mangungo alionesha udhaifu mkubwa sana Mkuu, usimtetee
 
Kati ya vitu alinisikitisha sana ni pamoja na hiki cha kuungana na mabeberu wanaoliibia Taifa letu!
Sina imani kabisa na uzalendo wake kwa nchi yetu.
Kwani kuna mabeberu wanoliibia taifa letu?
 
Mikataba ya kinyonyaji. Haina tofauti yeyote na yanayo husishwa na dole gumba la Chifu!
Mangungo hakuwa anajua kusoma na kuandika, ila nyie mnajua kusoma na kuandika na mnasaini bila hata kushikiwa bunduki.
 
Beberu amepewa kibali cha kupora na Waafrika wenzenu. Africa ya leo tofauti na ya Mangungo hakuna mahali beberu anaweza kuja kuchukua rasilimali kwa mabavu bila kuruhusiwa na wamiliki wa hizo rasilimali.
Wanachokiiba hao Watanzania wenzetu, ni kidogo sana kulinganisha na kinachoibwa na mabeberu. Japo mwizi ni mwizi tu awe wa ndani au wa nje
 
mangungo alionesha udhaifu mkubwa sana Mkuu, usimtetee
Unasumbuka na kina Mangungo ambao hawakujua better na ilikuwa ni offer they can not refuse (kubali kataa mali wanachukua) wakati hawa wa leo wanaingia mikataba huku wakijua fika kwamba wanauza nchi kwa kujiliwaza kwamba ni uwekezaji / kufungua nchi na wengine wakikopa willy nilly wakati mpaka vitukuu ndio vitalipia ufujaji wao wa leo ?
 
Chifu mangungo ni nani?

Naomba ninukuu kidogo kipande cha historia fupi kuhusu chifu Mangungo kutoka katika uzi wa ndugu humu Jf KILABA

"Mangungo simultaneously for all his people and Dr. Peters for alt his present and future associates hereby concluded a treaty of Eternal Friendship.

Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.

Dr. Karl Peters, in the name of the Society for German Colonization declares his willingness to take over the territory of the Sultan Mangungo with all rights for German Colonization subject to any existing suzerainty of Mwenyi Sagara.

In pursuance thereof, Sultan Mangungo hereby cedes all the territory of Msovero, belonging to him by inheritance or otherwise for all time, to Dr. Karl Peters, making over to him at the same time all his rights.

Dr. Karl Peters in the name of the Society for German Colonization undertakes to give special...attention to Msovero when colonizing Usagara.

This treaty has been communicated to the Sultan Mangungo by the interpreter Ramzan in a clear manner and has been signed by both sides, with the observation of the formalities valid in Usagara the Sultan on direct enquiry having declared that he was not in anyway dependent upon the Sultan of Zanzibar, and that he did not even know the existence of the latter.

Sgd. Dr. KARL PETERS
Sgd. MANGUNGO

This contract has been executed legally and made valid for all time before a great number of witnesses, we testify herewith:
Kwagakinga (mark);
Sultan Mangungo’s son of Golola (mark);
Sultan Mangungo’s second son of Draman (mark);
Graf Pfeil August Otto;
Mark of the intepreter Ramazan etc.
Dr. Karl Juhlke.
Msovero Usagara November 29, 1884.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, kwa Kiswahili unasomeka hivi:
Mangungo, Sultan wa Msovero katika Mwenyisagara, na Dk. Karl Peters. Mangungo sambamba na watu wake wote na Dk. Peters kwa niaba yake na washirika wake wengine wajao kwa pamoja wanaweka mkataba wa Urafiki wa Kudumu.

Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.

Dk. Karl Peters, kwa niaba ya jina la Umoja wa Ukoloni wa Ujermani anatangaza dhamira yake ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.

Katika kutekeleza hilo, Sultan Mangungo anakabidhi himaya yote ya Msovero, inayomilikiwa na yeye mwenyewe kwa urithi au kwa namna yoyote ile kwa nyakati zote, kwa Dk. Karl Peters, na wakati huo huo kumkabidhi haki zake zote.

Dk. Karl Peters kwa niaba ya Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani anakusudia kuweka mkazo maalum kwa eneo la Msovero wakati wa kuitawala Usagara.

Mkataba huu umewasilishwa kwa Sultan Mangungo na mkalimani Ramzan katika dhana ya wazi kabisa na umesainiwa na pande zote, kwa kuzingatia taratibu zilizopo katika Usagara, Sultan baada ya kuhojiwa moja kwa moja alikiri kwamba hakuwa na ushirika ama kutegemea kwa namna yoyote Sultan wa Zanzibar, na kwamba hakuwa hata akimfahamu.

Imesainiwa. Dk. KARL PETERS
Imesainiwa. MANGUNGO

Mkataba huu umefanyika kihalali kabisa na umehuishwa kwa nyakati zote mbele za mashahidi wengi, ambao tunakiri hapa:
Kwagakinga (dole gumba);
Golola mtoto wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Draman mtoto wa pili wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Graf Pfeil August Otto.
Dole gumba la mkalimani Ramazan etc.
Dk. Karl Juhlke.
Msovero Usagara Novemba 29, 1884.
Mmmmh!!

Tumetoka mbali
Asante Mkuu
 
Beberu amepewa kibali cha kupora na Waafrika wenzenu. Africa ya leo tofauti na ya Mangungo hakuna mahali beberu anaweza kuja kuchukua rasilimali kwa mabavu bila kuruhusiwa na wamiliki wa hizo rasilimali.
Kweli kabisa Mkuu
 
Endapo Tanzania tungalikuwa na utaratibu wa kufanya "corronation" kwa marais wetu baada ya kipindi fulani kupita baada ya uchaguzi. Na pia Rais mteule achunguzwe na kupewa jina kupitia tabia yake kuendana na wafalme waliopita na kutawala sehemu mbalimbali za Tanganyika.
Kati ya viongozi ambao hawakupaswa kuandikwa hata kwenye vitabu vya kihistoria ni chifu Mangungo wa Msovero maana ni kielelezo kibaya sana na cha aibu kwa Taifa letu.
Siku nikifanikiwa kuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi, nitapiga marufuku kabisa kwa viongozi wote wenye kariba ya Chifu Mangungo kuwekwa kwenye historia ya nchi yetu.

Watoto wetu wanapaswa kufundishwa habari za kina Chifu Mkwawa wa Iringa, Chifu Mirambo wa Tabora, Chifu Isike n.k.

Hiyo itawafanya na wao kuwa na moyo wa uzalendo kama ya hao mashujaa niliowataja hapo juu.

Huenda labda kwa kufanya hivyo tukafanikiwa kuwa na viongozi wazalendo watakaolivusha Taifa letu, kututoa tulipo, na kutupeleka sehemu nzuri zaidi.

Naomba kuwasilisha.
Ninaamini kabisa majina ya marais wetu ukimuondoa Mwl. Nyerere, kutokana na mikataba waliyoliingiza taifa letu, pengine yote yangalibaki kuwa na haiba ya kimangungo yaani tungalipata safu ya Mangungo I, Mangungo II,......., Mangungo V na wote wakitoka CCM.
 
Endapo Tanzania tungalikuwa na utaratibu wa kufanya "corronation" kwa marais wetu baada ya kipindi fulani kupita baada ya uchaguzi. Na pia Rais mteule achunguzwe na kupewa jina kupitia tabia yake kuendana na wafalme waliopita na kutawala sehemu mbalimbali za Tanganyika.Ninaamini kabisa majina ya marais wetu ukimuondoa Mwl. Nyerere, kutokana na mikataba waliyoliingiza taifa letu, pengine yote yangalibaki kuwa na haiba ya kimangungo yaani tungalipata safu ya Mangungo I, Mangungo II,......., Mangungo V na wote wakitoka CCM.
Kwa hiyo kuweka vizuri tuko na mangungo wa 5 (mangungo v)?!
😁😁😁😁😁
Labda atakuwa the fourth maana mwenzao mmoja alikuwa mkali sana linapokuja suala la mikataba ya ovyo ovyo
 
Kwa hiyo kuweka vizuri tuko na mangungo wa 5 (mangungo v)?!
😁😁😁😁😁
Labda atakuwa the fourth maana mwenzao mmoja alikuwa mkali sana linapokuja suala la mikataba ya ovyo ovyo
 

Attachments

  • Rais_Magufuli_kuhusu_Ufisadi_na_Tanzania_kuwa_Shamba_la_Bibi_|Mar_20,_2016_|(144p).mp4
    1.3 MB
Kati ya viongozi ambao hawakupaswa kuandikwa hata kwenye vitabu vya kihistoria ni chifu Mangungo wa Msovero maana ni kielelezo kibaya sana na cha aibu kwa Taifa letu.
Siku nikifanikiwa kuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi, nitapiga marufuku kabisa kwa viongozi wote wenye kariba ya Chifu Mangungo kuwekwa kwenye historia ya nchi yetu.

Watoto wetu wanapaswa kufundishwa habari za kina Chifu Mkwawa wa Iringa, Chifu Mirambo wa Tabora, Chifu Isike n.k.

Hiyo itawafanya na wao kuwa na moyo wa uzalendo kama ya hao mashujaa niliowataja hapo juu.

Huenda labda kwa kufanya hivyo tukafanikiwa kuwa na viongozi wazalendo watakaolivusha Taifa letu, kututoa tulipo, na kutupeleka sehemu nzuri zaidi.

Naomba kuwasilisha.
Hebu tuelimishane, tatizo la Chifu Mangungu lilikuwa nini?
 
Inasikitisha sana..
Kiongozi mmoja aliwahi kusema, iko siku makaburi ya viongozi kama hao yatachapwa viboko!
Mimi nadhani tusisubiri hadi wafe ndo tukawatandike. Inabidi watandikwe wakiwa bado hai ili na wengine wapate kujifunza.
Nenda katangulie kuchapa kaburi la aliyetoa hiyo kauli maana naye ametuachia matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na kugawa nchi. Sasa wananchi wa nchi moja wanatukanana kisa ukanda, mara utasikia usioe mwanamke wa kaskazini. Unafikiri nani kalete haya yote? Huyo mwendawazimu wako.
 
Kati ya viongozi ambao hawakupaswa kuandikwa hata kwenye vitabu vya kihistoria ni chifu Mangungo wa Msovero maana ni kielelezo kibaya sana na cha aibu kwa Taifa letu.
Siku nikifanikiwa kuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi, nitapiga marufuku kabisa kwa viongozi wote wenye kariba ya Chifu Mangungo kuwekwa kwenye historia ya nchi yetu.

Watoto wetu wanapaswa kufundishwa habari za kina Chifu Mkwawa wa Iringa, Chifu Mirambo wa Tabora, Chifu Isike n.k.

Hiyo itawafanya na wao kuwa na moyo wa uzalendo kama ya hao mashujaa niliowataja hapo juu.

Huenda labda kwa kufanya hivyo tukafanikiwa kuwa na viongozi wazalendo watakaolivusha Taifa letu, kututoa tulipo, na kutupeleka sehemu nzuri zaidi.

Naomba kuwasilisha.
Wewe ni mpumbavu mmoja unayeendeshwa na hisia au hujajipa nafasi ya kutafakari Chief Mangungo alifanya nini.
Hata leo hii wazungu wanapewa mikataba ya uwekezaji tena ya sasa ni mibaya zaidi kuliko huo wa Mangungo.

Hawa akina Mkwawa wana mambo mengi machafu na maovu waliyowatendea watu wao kuliko ushujaa unaokuzwa ili kupamba tawala zao.

Nadhani ukoloni ilikuwa lazima uje ili kutunasua na tawala zilizoongozwa na wachawi.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Nyaraka za Pandora
zinaonyesha utajiri uliofichwa, ukwepaji wa kodi na, wakati mwingine, utakatishaji fedha unaofanywa na baadhi ya matajiri na wenye nguvu duniani-na makaburu!
Kwa lugha nyingine ni sawa na "kutuibia?"
kaburu sifa kuu ni ubaguzi hasa kwa misingi ya rangi. Kaburu kapora mali ya nani. Afika kusini ni kwao maana mababu zao walihamia kule miaka mingi sana nyuma kabla hata blacks hawajajua hata maana ya nchi.
 
Mabeberu wameweka mizizi yao hadi chumbani mwa nchi(kuna agent wa wabeberu) .so ukienda tofauti nao huwezi kusurvive yu wapi? Gadaffi,JPM na wengine wengi walioenda tofauti na mabeberu.nchi yulipata mwamba JPM tukamtukana na kumkejeli kwa matusi hadi baada ya kifo chake ambaye alijitolea kutetea Taifa alidiriki kuumiza wa2 na wengine hadi kufa aliowaona wanakwamisha safari yake ya kulikomboa Taifa dhidi ya mabeberu na agent wao,bado hatukumwelewa na kumuuita muuaji.mwacheni mama wa watu atete uhai wake na kujikusanyia chake muda wake uishe ale maisha na familia yake(kama mulichomfanyia mtangulizi wake amejionea mwenyewe ivi hata ungekuwa wewe ungapata wapi? Moyo wa kuwatetea na kurisk maisha yako)
Hivi unajionaje unavyosema Magufuli alikuwa anatetea Taifa, alikuwa anaitetea dhidi ya nani. Hakuna mtu mwovu na wa hovyo kutokea nchi hii km Magufuli alikuwa mwongo sana na miongoni mwa alioweza kuwadanganya ni zuzu km wewe. Aliiharibun nchi hii, aligawa nchi ndiyo kumejitokeza kauli za kibaguzi ambazo hazijawahi kuwepo tangia nchi ipate uhuru. Leo utasikia usioe kaskazini n.k Yule alikuwa kaburu mweusi usitake kutukumbusha.
 
Back
Top Bottom