Akili za Chifu Mangungo wa Msovero

mangungo alionesha udhaifu mkubwa sana Mkuu, usimtetee
 
Kati ya vitu alinisikitisha sana ni pamoja na hiki cha kuungana na mabeberu wanaoliibia Taifa letu!
Sina imani kabisa na uzalendo wake kwa nchi yetu.
Kwani kuna mabeberu wanoliibia taifa letu?
 
Mikataba ya kinyonyaji. Haina tofauti yeyote na yanayo husishwa na dole gumba la Chifu!
Mangungo hakuwa anajua kusoma na kuandika, ila nyie mnajua kusoma na kuandika na mnasaini bila hata kushikiwa bunduki.
 
Beberu amepewa kibali cha kupora na Waafrika wenzenu. Africa ya leo tofauti na ya Mangungo hakuna mahali beberu anaweza kuja kuchukua rasilimali kwa mabavu bila kuruhusiwa na wamiliki wa hizo rasilimali.
Wanachokiiba hao Watanzania wenzetu, ni kidogo sana kulinganisha na kinachoibwa na mabeberu. Japo mwizi ni mwizi tu awe wa ndani au wa nje
 
mangungo alionesha udhaifu mkubwa sana Mkuu, usimtetee
Unasumbuka na kina Mangungo ambao hawakujua better na ilikuwa ni offer they can not refuse (kubali kataa mali wanachukua) wakati hawa wa leo wanaingia mikataba huku wakijua fika kwamba wanauza nchi kwa kujiliwaza kwamba ni uwekezaji / kufungua nchi na wengine wakikopa willy nilly wakati mpaka vitukuu ndio vitalipia ufujaji wao wa leo ?
 
Mmmmh!!

Tumetoka mbali
Asante Mkuu
 
Beberu amepewa kibali cha kupora na Waafrika wenzenu. Africa ya leo tofauti na ya Mangungo hakuna mahali beberu anaweza kuja kuchukua rasilimali kwa mabavu bila kuruhusiwa na wamiliki wa hizo rasilimali.
Kweli kabisa Mkuu
 
Endapo Tanzania tungalikuwa na utaratibu wa kufanya "corronation" kwa marais wetu baada ya kipindi fulani kupita baada ya uchaguzi. Na pia Rais mteule achunguzwe na kupewa jina kupitia tabia yake kuendana na wafalme waliopita na kutawala sehemu mbalimbali za Tanganyika. Ninaamini kabisa majina ya marais wetu ukimuondoa Mwl. Nyerere, kutokana na mikataba waliyoliingiza taifa letu, pengine yote yangalibaki kuwa na haiba ya kimangungo yaani tungalipata safu ya Mangungo I, Mangungo II,......., Mangungo V na wote wakitoka CCM.
 
Kwa hiyo kuweka vizuri tuko na mangungo wa 5 (mangungo v)?!
😁😁😁😁😁
Labda atakuwa the fourth maana mwenzao mmoja alikuwa mkali sana linapokuja suala la mikataba ya ovyo ovyo
 
Kwa hiyo kuweka vizuri tuko na mangungo wa 5 (mangungo v)?!
😁😁😁😁😁
Labda atakuwa the fourth maana mwenzao mmoja alikuwa mkali sana linapokuja suala la mikataba ya ovyo ovyo
 

Attachments

  • Rais_Magufuli_kuhusu_Ufisadi_na_Tanzania_kuwa_Shamba_la_Bibi_|Mar_20,_2016_|(144p).mp4
    1.3 MB
Hebu tuelimishane, tatizo la Chifu Mangungu lilikuwa nini?
 
Inasikitisha sana..
Kiongozi mmoja aliwahi kusema, iko siku makaburi ya viongozi kama hao yatachapwa viboko!
Mimi nadhani tusisubiri hadi wafe ndo tukawatandike. Inabidi watandikwe wakiwa bado hai ili na wengine wapate kujifunza.
Nenda katangulie kuchapa kaburi la aliyetoa hiyo kauli maana naye ametuachia matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na kugawa nchi. Sasa wananchi wa nchi moja wanatukanana kisa ukanda, mara utasikia usioe mwanamke wa kaskazini. Unafikiri nani kalete haya yote? Huyo mwendawazimu wako.
 
Wewe ni mpumbavu mmoja unayeendeshwa na hisia au hujajipa nafasi ya kutafakari Chief Mangungo alifanya nini.
Hata leo hii wazungu wanapewa mikataba ya uwekezaji tena ya sasa ni mibaya zaidi kuliko huo wa Mangungo.

Hawa akina Mkwawa wana mambo mengi machafu na maovu waliyowatendea watu wao kuliko ushujaa unaokuzwa ili kupamba tawala zao.

Nadhani ukoloni ilikuwa lazima uje ili kutunasua na tawala zilizoongozwa na wachawi.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Nyaraka za Pandora
zinaonyesha utajiri uliofichwa, ukwepaji wa kodi na, wakati mwingine, utakatishaji fedha unaofanywa na baadhi ya matajiri na wenye nguvu duniani-na makaburu!
Kwa lugha nyingine ni sawa na "kutuibia?"
kaburu sifa kuu ni ubaguzi hasa kwa misingi ya rangi. Kaburu kapora mali ya nani. Afika kusini ni kwao maana mababu zao walihamia kule miaka mingi sana nyuma kabla hata blacks hawajajua hata maana ya nchi.
 
Hivi unajionaje unavyosema Magufuli alikuwa anatetea Taifa, alikuwa anaitetea dhidi ya nani. Hakuna mtu mwovu na wa hovyo kutokea nchi hii km Magufuli alikuwa mwongo sana na miongoni mwa alioweza kuwadanganya ni zuzu km wewe. Aliiharibun nchi hii, aligawa nchi ndiyo kumejitokeza kauli za kibaguzi ambazo hazijawahi kuwepo tangia nchi ipate uhuru. Leo utasikia usioe kaskazini n.k Yule alikuwa kaburu mweusi usitake kutukumbusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…