Akili za Maisha na Akili za Darasani

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
NImesikia hili swala mara nyingi sana yaani akili za darsani na za maisha....!

Je Akili za darasani ni zipi na za Maisha ni zipi!?

Naomba Kila Mtu Ajibu kwa mtazamo wake...ili Kila mmoja again Knowledge!
 
Akili za darasani ni kama hizi ulizoziweka kwenye huu uzi wako.
 
Akili za maisha ni nyingi sana wewe unazungumzia akili zipi
 
akili za darasani ni ule uwezo wa kufaulu masomo katika mitihani na akili za maisha ni ule uwezo wa kutumia ufahamu wako kuweza kutatua changamoto za maisha. Si kila aliyefaulu darasani anaweza kufaulu katika maisha. Ndio maana unakutana na mtu hajasoma sana lakini ameweza kuwa na maisha mazuri!
 

Maisha mazuri ni yapi? Asilimia ngapi ya waliosoma wana maisha mazuri na asilimia ngapi ya wasiosoma wana maisha mazuri?
 
AKILI YA DARASANI.

Ni namna ambavyo mtu anakuwa na elimu kuhusiana na masuala aliyesomea akiwa darasani, mfano uhandisi, ualimu, udaktari, n.k

Nje ya hapo hatoweza kufanya au kujiongeza kwa chochote kitu akiwa amekosa hiyo elimu ya darasani.


AKILI YA MTAANI.
ni ule uwezo wa mtu kuwa na akili ya ziada katika kufanya jambo au kazi Fulani na kumletea manufaa mbeleni, mfano inaweza ikawa ni kipaji cha muziki, kipaji cha kucheza mpira, au kufanya kazi ndani ya jamii kama kuuza duka la spea n.k
hii inakuwa hujapitia shule kupata elimu ya juu.
 
kuwa na Maisha mazuri ndio Akili za Maisha?
 
well
 
Akili ya Darasani ni mimi nikiwa sekondari, nikijitahidi kuwa kwanza. Waliofeli feli huko kwa sasa wana biashara zao wameoa wana familia wanaendelea vizuri.

Akili za Maisha ni pale nilipomaliza chuo na amana ajira. Nikaamua kujiajiri na kuwa mfanyabiashara, elimu ya form four ilinitosha kabisa kufanya haya. Sasa nimetambua shule inakuaandaa uajiriwe, kama hujapata ajira utachanganyikiwa kama hujijali..
 
Elimu ya Maisha ni pale kaka alipokutana na Taasisi ya kimataifa inayowezesha maswala kilimo hapa nchini, kwa ajili ya ucheshi na utundu akapata dhamana ya kuwa Entrepreneur Program Coordinator wakati alisomea Linguistics.. Ilibidi afanye kwa kujifunza na kupata uzoefu.
 
hahahaa
 
Akili za maisha ni zile zinazomwezesha mtu kutengeneza maisha au kuifanya dunia yake sehemu nzuri ya kuishi!

Akili ya darasani ni ile inayokuwezesha kufanya vizuri darasani na kutengeza vyeti vyako uwe na GPA kubwa nk.
 
Akili ni akili tu,inategemea unaitumiaje kulingana na mazingira. Ukiwa shule ukitumia vizuri akili itakuletea hilo neno(akili ya darasani).Ukiwa mtaani ukitumia akili vizuri bas utakuwa na akili ya maisha
Hata hapa jf ukiandika upuuzi,utakuwa na akili za kipuuzi.
 
Well said mkuu.
Maisha ni chochote unachokifanya na akili ya maisha ni chochote unachokifikilia kwa Lengo lolote.itakuwa nzur kama itakupa matokeo chanya na kinyume chake ni sahihi...kama shule sio part ya maisha basi itakuwa na akili yake..[HASHTAG]#Nguvu[/HASHTAG] ya Elimu inaonekana pale Elimu inapotumika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…