Akili za mashabiki wa timu ya Yanga na viongozi wao zinaendana

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Sijapata kuona watu waliokosa akili kama mashabiki wa Yanga. Nimesikitika sana pamoja na kuwa ni mshabiki wa Yanga lakini kamwe hakuna na kusitarajie mafanikio kwa Yanga kwa aina hii ya mashabiki waliokuwa wapumbavu kiasi hiki na pia kwa viongozi wasiokuwa na mikakati na mipango ili kutimiza malengo.

Viongozi wa Yanga wanachofanya ni kuvunja mabenchi ya ufundi ili kufichia madhaifu yao. Lakini ukweli ni kwamba kwa mfumo wa uendeshaji huu wa timu + uswahili + ukilaza wa washabiki basi sio ajabu Simba ikichukua kombe hata zaidi ya miaka 20

Viongozi wa Yanga hawana wanachojua kukifanya zaidi ya kusajili wachezaji wapya na kuvunja mabenchi ya ufundi kwa mihemko tu kila msimu. yule kocha aliyetimuliwa kisa kuisema Yanga vibaya, alikuwa sahihi sana sema ndio kawaida ya ukweli huwa unauma.

Washabiki wakisema tu hatumtaki fulani basi katimuliwa, tumeona kwanzia kwa Zahera, Kisha yule aliyeita Yanga manyani na huyu Kaze pia washabiki wakishaanza maneno tu basi kinachofuata kocha ni kutimuliwa hapo inaonesha wazi kuwa viongozi hawana msimamo pili wanacheza ngoma ya mashabiki ilimradi tu mambo yasivuke kwao (kuficha madhaifu yao)

Mashabiki nao walivyowapumbavu Kuna mambo ya msingi ambayo viongozi wanapaswa kuwajibishwa ikiwemo swala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa timu mchakato umekuwa kimya mpaka sasa. Mpira ni pesa, mikakati, na mipango kufikia malengo. Je wanashindwa nini kuwapa timu wawekezaji?

Pili kuhusu sajili wanazofanya, ni wachezaji kadhaa tu ndio wanaokuja kwa matakwa ya kocha lakini wengi wao wanasajili viongozi na machezaji ni magalasa kabisa yasiyofaa kuchezea Yanga je kwanini nao wasijiwajibishe kwa kujiuzuru nafasi zao?

Uhuni na uswahili wanaofanya kwa mashabiki wa Yanga kama vile mashabiki ni watoto wadogo (kesi ya Morrison) Mwakalebela alikuwa kila mara anaita waandishi wa habari kuzungumza kuhusu kesi hewa ya Morrison, je kwanini viongozi hawaajibishwi?

Yanga imekosa dira hakuna mipango yakueleweka ambayo mpaka sasa imefanyika ili kuifanya Yanga isimame kama timu na kama brand. Wanaanzisha jambo kisha hakuna kinachoendelezwa hata taarifa ya maendeleo hakuna (uwanja wa Kigamboni) unaonesha chumba cha mfano badala ya kuonesha ujenzi wa uwanja wa mazoezi.

Mashabiki endeleeni kupigaga kelele juu ya makocha hawafai, waamuzi hawafai kila mara bila kufikiria kwa makini mzizi au chimbuko la matatizo ya Yanga ni wapi.
 
Ni kweli tupu.

Mashabiki wengi wa yanga pamoja na viongozi wao ni mbumbumbu sana.

Kama mtu mwenye akili timamu, unawezaje kuamini headlines za magazeti na wachambuzi maandazi kuwa eti Tusila analingana na Miquesone? Au kulinganisha level ya Simba na yanga kisha mnajiona eti mpo bora sana!

Hapo Ndipo uto mnakwama.

Msijilinganishe na Simba. Jengeni timu yenu. Acheni kudai 20B kwa Mo mkiamini sisi wanasimba ni kama mlivyo vilaza ninyi wa yanga.Sisi tunaangalia matokeo uwanjani.
 
Msikilize mtaalam hapa
Mwalimu Kashasha kaongea ukweli mtupu. Dkt Msola sijui elimu yake inamsaidia nini. Yaani mtu msomi mzima lakini unashindwa kupanga mambo kisomi unaishia kusikiliza maneno ya mashabiki halafu unafukuza kocha unaanza na upya.

Halafu msimu mpya ukianza unaacha wachezaji saba halafu unasajili wapya.
 
All in all mashabiki wa utopolo ni hamnazo lakini uwekezaji wa GSM nikama ni wamashaka mashaka wanasita sana kutoa pesa
 
All in all mashabiki wa utopolo ni hamnazo lakini uwekezaji wa GSM nikama ni wamashaka mashaka wanasita sana kutoa pesa
GSM hajawekeza Yanga, mkataba wake na Yanga upo kwenye jezi tu hayo mengine anayoyafanya anafanya kama hisani tu. Timu inaendeshwa kihuni huni tu kwakifupi hakuna aliyekuwa serious na mwelekeo wa hili timu.

Viongozi wapo wapo tu sijui akili yao inawaza mafanikio ya ghafla bila kujijenga, kupanga na kuweka misingi sahihi ya kufikia unapopataka.
 
Kocha wa mataji akatua Yang usiku na file zima la Simba! Ila yanga huwa wanadanganywa kinoma ,afu yanga ikianza kufanya vibaya utawasikia washambiki wa yanga, wacha ituuwe kauli za kindezi yani ni utopolo mtu.
 

Msolla hana ujanja. Anatafuta mbinu ya kulinda ajira yake, anatumia mbinu ya kufukuza makocha ili aonekane yeye mwema hausiki na timu kufungwa.
 
Tulishuhudia kwenye vyombo vya habari Boss kutoka GSM akiwa huko Espanyora kua ametoka ku sign deal na club moja hoko espanyora ,huu mchakato haujaleta mafanikio yoyote hapo jangwa? That why nasema hata uwekezaji wa GSM ni hamna kitu janja janja
 
Waacheni wale viongozi waongoze klabu.

Kocha Kaze anashindwaje kuwapa nafasi mtu kama Waziri jr anang'ang'ana na wakina nchimbi na firston washambuliaji butu.

Kocha gani anakosa first 11 kwenye timu?
Kocha gani ajui kufanya sub?
Kaze kashindwa hata kuijenga timu ionekane inacheza mfumo upi,4,4,2-4,3,3 ama mfumo upi?
Yanga wakiwa wanacheza unaona kabisa ni juhudi za wachezaji binafsi na sio muunganiko wa kiufundi kama timu.
 
Kila kona ni thread za yanga tu!

Wakuu, wapuuzeni hawa yanga hawajui wanachokitaka msimu huu
 
Waacheni wale viongozi waongoze klabu.

Kocha Kaze anashindwaje kuwapa nafasi mtu kama Waziri jr anang'ang'ana na wakina nchimbi na firston washambuliaji butu...
Hayo yanaonekana baada ya mzunguko wa pili? Mzunguko wa kwanza hakuna aliyeona kuwa wachezaji wanacheza kwa juhudi zao bali ni Kazelona ndio inafanya kazi. Ndio aina ya mashabiki wa mpira wa Tanzania tulivyo wanafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…