Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Sijapata kuona watu waliokosa akili kama mashabiki wa Yanga. Nimesikitika sana pamoja na kuwa ni mshabiki wa Yanga lakini kamwe hakuna na kusitarajie mafanikio kwa Yanga kwa aina hii ya mashabiki waliokuwa wapumbavu kiasi hiki na pia kwa viongozi wasiokuwa na mikakati na mipango ili kutimiza malengo.
Viongozi wa Yanga wanachofanya ni kuvunja mabenchi ya ufundi ili kufichia madhaifu yao. Lakini ukweli ni kwamba kwa mfumo wa uendeshaji huu wa timu + uswahili + ukilaza wa washabiki basi sio ajabu Simba ikichukua kombe hata zaidi ya miaka 20
Viongozi wa Yanga hawana wanachojua kukifanya zaidi ya kusajili wachezaji wapya na kuvunja mabenchi ya ufundi kwa mihemko tu kila msimu. yule kocha aliyetimuliwa kisa kuisema Yanga vibaya, alikuwa sahihi sana sema ndio kawaida ya ukweli huwa unauma.
Washabiki wakisema tu hatumtaki fulani basi katimuliwa, tumeona kwanzia kwa Zahera, Kisha yule aliyeita Yanga manyani na huyu Kaze pia washabiki wakishaanza maneno tu basi kinachofuata kocha ni kutimuliwa hapo inaonesha wazi kuwa viongozi hawana msimamo pili wanacheza ngoma ya mashabiki ilimradi tu mambo yasivuke kwao (kuficha madhaifu yao)
Mashabiki nao walivyowapumbavu Kuna mambo ya msingi ambayo viongozi wanapaswa kuwajibishwa ikiwemo swala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa timu mchakato umekuwa kimya mpaka sasa. Mpira ni pesa, mikakati, na mipango kufikia malengo. Je wanashindwa nini kuwapa timu wawekezaji?
Pili kuhusu sajili wanazofanya, ni wachezaji kadhaa tu ndio wanaokuja kwa matakwa ya kocha lakini wengi wao wanasajili viongozi na machezaji ni magalasa kabisa yasiyofaa kuchezea Yanga je kwanini nao wasijiwajibishe kwa kujiuzuru nafasi zao?
Uhuni na uswahili wanaofanya kwa mashabiki wa Yanga kama vile mashabiki ni watoto wadogo (kesi ya Morrison) Mwakalebela alikuwa kila mara anaita waandishi wa habari kuzungumza kuhusu kesi hewa ya Morrison, je kwanini viongozi hawaajibishwi?
Yanga imekosa dira hakuna mipango yakueleweka ambayo mpaka sasa imefanyika ili kuifanya Yanga isimame kama timu na kama brand. Wanaanzisha jambo kisha hakuna kinachoendelezwa hata taarifa ya maendeleo hakuna (uwanja wa Kigamboni) unaonesha chumba cha mfano badala ya kuonesha ujenzi wa uwanja wa mazoezi.
Mashabiki endeleeni kupigaga kelele juu ya makocha hawafai, waamuzi hawafai kila mara bila kufikiria kwa makini mzizi au chimbuko la matatizo ya Yanga ni wapi.