Jaman mie nahisi sijui ndio maumbile au vp,
Mie ilinitokea hivi;Kwetu hatuna kaka mkubwa kaka yetu ni mdogo wangu wa pili asa siku moja akanikuta natoka church niko na mkaka tunatembea njian tunaongea alipotufikia akanisalimia akamsalimia na yule mkaka alafu eti akasimama akamcheki kiaina alafu akaondoka kumbe kaenda kusimama mahali mie nipokatiza njia ya kwenda hm na yule kaka akaondoka zake kumbe eti alimfata yule kaka na kuanza kumhoji kuhusu mie yule kaka akamwelewesha kuwa ss ni marafiki tu,eti mdogo wangu akamwambia acheze mbali na mie lol!
Nilipojua nilimwita mdogo wangu nikaongea naye kwa upendo na kumshukuru kwa kunijali na kumtoa wasiwasi kuwa niko makin sana na kwa umri nilionao namudu kupambana na wanaume kwa hiyo asiwe anaingilia kwa namna yoyote nitakapo hitaji msaada wake basi nitamwambia,akanielewa natangu siku hiyo wala hana habari hata akiniona na mtu.