...akililia wembe mpe...!

...akililia wembe mpe...!

Hivi kumbe mtu kuitwa mtoto wa fulani ni lazima biological proof? Vipi kuhusu watoto adopted? Au inakuwa vipi kama mhusika alikubali kuoa mke mwenye mtoto tayari, ina maana mtoto huyo hutengwa? Au wale ambao wake zao hupandikizwa mimba kwa mbegu za mwanamke na/au mwanaume asiye mumewe, ina maana watoto wa zao hilo huwa hawapati hizo viza? Kuna watu kadhaa ninaowafahamu ambao nasikiaga huwa hawana uwezo wa kuzaa, lakini waliendaga South Africa na Ufaransa wakarudi na watoto wanaoitwa wa kwao, hapo DNA najua itagoma, sasa biological proof ya ubaba/umama inakuwaje, na ina maana watoto hao huko ughaibuni wanabaguliwa?

Naomba kuelimishwa
Hivi kweli walitumia vigezo gani hapo Ubalozini,kwanini walitaka uhalali wa mtoto na hakika alikuwa na birthcertificate,au mwenyewe alikuwa na wasiwasi ??

...Sijui kwa balozi nyingine, lakini masharti ya ubalozi wa uingereza kwa 1st time settlement visa ni;
In January 1991 the UK government introduced a scheme which uses DNA testing to help resolve relationship disputes in immigration applications. These relationship tests are often more complex than standard paternity cases and the analysis and reporting therefore sometimes takes a little longer.

Cellmark is the only company contracted to the UK Border Agency's UKvisas scheme to provide all of their DNA relationship testing. Our results are accepted by United Kingdom and United States immigration departments as well as by other government immigration departments.

source; http://www.cellmark.co.uk/dna_testing/immigration_dna_testing.php
 
MWISHO WA UBAYA NI AIBU!
Jamaa si alitaka kumfanyia mkewe ubaya kwa kwenda kinyemela kuoa? Sasa kiko wapi?
Mbu unataka kumshauri vipi zaidi ya kumwambia ukweli?

...aaah jamani, dini yake inamruhusu wanne...
na siunajua tena jamaa zetu hawa wa Kipemba!
...Hawaachi asili!
 
Malipo ni hapa hapa duniani, kesho akhera hesabu tu! Serves him right! naye huyo mwanadada kakosa na majuu pia. hamna cha gharama hapo, amelipia uzinzi wake! asiwe ameambukizwa ngoma basi, hiyo gharama itakuwa child play!

Mbu...u dont need to feel sorry for your buddy unless u were part of the plan! hebu twambie how do u feature in this?

...mnh, shishi unanitega sasa...😀
basi tu, namuonea huruma kwa yaliyomkuta!

Maisha yenyewe ughaibuni boksi, boski na yeye halafu
mlimbwende anamkatiili kiasi hicho?..

mnh wanawake nanyi mna roho ngumu!!!
 
To hell with all ze costs...haendi mtu Ughaibuni, hata kama kaogaje au amepata hiyo Viza!...Cheating about a child is full intolerable...Wa nini mtu wa hivyo?

Bahati si yake...We Chapa zako malapa Ulaya, mwache huyo mzinzi aendelee kunyonyoa nyau Bongo!

Alaaa!

Mzinzi mwanamue aliyemuacha mkewe akaenda kuvamia mlupo (naamini demu alikuwa single) ! Hakuna cha ushauri hapo zaidi ya kumrudia mkewe wa ndoa na akome kudandia treni kwa mbele.
 
Huyo jamaa yako alijitakia mwenyewe ... kwanza inaonyesha mke mdogo alikaa Bongo kwa muda mrefu akiwa peke yake. Pili inawezekana huyo jamaa alijisahau (kimawasiliano) kwa kuwa alikuwa na mke mkubwa, so hana upweke na wala hawezi kum-miss sana mke mdogo.

Dunia ya leo unaoa mitala halafu mke mdogo damu bado inachemka anataka shughuli muda wote, unamuacha akae peke yake miezi 6 au zaidi, na anajua wazi kwamba huko uliko wewe unapata huduma kama kawaida, kwanini ajitese kukusubiri? Wakija vijana wasiotaka makubwa anajirusha na matokeo yake ndiyo hayo. Hakuna mwanamke wa siku hizi ambaye yuko tayari kusubiri huduma ya ndoa ya mgao, likizo mpaka likizo, na likizo yenyewe mara moja kwa mwaka. Why starve? While your husband is having some with bi mkubwa?

Jamani hayo maisha waliishi wazee wetu na zama hizo ngono haikuwa starehe ilikuwa inatumika kwa ajili ya uzazi. Siku hizi ngono ni starehe na ndio maana manjonjo kibao ili kukoleza shughuli yenyewe.

Mwanamke gani wa leo ambaye atakaa kusubiri mume aje kumuona once in a yr na aachwe na mimba?

Ukishaoa mitala na kama kuna distance kubwa kutoka kwa mke mmoja kwenda kwa mwingine, basi uwe tayari kuibiwa. Unadhani kwanini wazee wa zamani walikuwa wanasema kwamba, "Kitanda hakizai haramu"? Kwa kuwa walikuwa wanajua kuna kuibiwa, na hasa kama mke kaachwa miezi 6 au mwaka mzima peke yake, ukikuta mkeo ni mjamzito wala hutakiwi kuuliza mimba ni ya nani? Bali ni kuwajibika kuitunza mpaka na mtoto.

Jamaa yako alitakiwa aoe na kuondoka na mke wake mara baada ya ndoa au asichukue zaidi ya miezi 6 ku-process maswala ya uhamiaji. Sasa jamaa kaacha mke mdogo peke yake, alitegemea nani amliwaze? Halafu mke mdogo aki-cheat wala haimuumi sana kwa kuwa anajua na mume wake anapata huduma kila siku.

Huyo jamaa kukaa kwake UK hakujamkomboa, maana naona anaishi maisha ya kijima, hata kama dini inakuruhusu, unatakiwa kutumia akili na kujiuliza kwa mazingira ya dunia ya leo unaweza kuacha mke mdogo miezi 6 au mwaka? Kama ni mke pekee inawezekana, ila siku akigundua kwamba una-cheat huko uliko na yeye ataanza kujirusha. Kwa mke wa mitala, hasubiri kugundua maana ana uhakika kwamba unapata huduma kwa mke mkubwa, so na yeye ataenda kusaka huduma kwa "mume mdogo".
 
Mzinzi mwanamue aliyemuacha mkewe akaenda kuvamia mlupo (naamini demu alikuwa single) ! Hakuna cha ushauri hapo zaidi ya kumrudia mkewe wa ndoa na akome kudandia treni kwa mbele.

Kwenye uislam kama mwanaume kafunga ndoa kwa Sheikh, hakuna uzinzi tena. Labda kosa la Ustaadh lilikuwa ni kwenda kuoa mke mdogo bila ridhaa ya bi mkubwa.

Kiutaratibu, kabla ya kwenda kuoa mke mwingine lazima uombe ridhaa ya mke mkubwa na utoe sababu za kueleweka kulingana na imani ya kiislam. Mke mkubwa akiridhia ndipo unakwenda kuoa na kuna wake wakubwa wengine ambao hupewa jukumu la ku-recommend/kumtafuta huyo bi mdogo.

Ni kweli ushauri kwa sasa ni too late, ila akubali tu kwamba mtoto ni wa kwake kwa kuwa kitanda huwa hakizai haramu. Hayo mengine yaliyojitokeza ni bahati mbaya na anatakiwa kuwa makini kama alikuwa na mpango wa kuoa mke wa 3 na wa 4. Pia na wengine watajifunza kutokana na makosa yake, labda itafika mahali wataona ndoa za mitala hazina maana tena.
 
...Sijui kwa balozi nyingine, lakini masharti ya ubalozi wa uingereza kwa 1st time settlement visa ni;

ok ,thanks kwa information hizi,ila sikumbuki kama mtoto wangu alifanya hivi wakati walivyonijoin.
 
...aaah jamani, dini yake inamruhusu wanne...
na siunajua tena jamaa zetu hawa wa Kipemba!
...Hawaachi asili!

sasa kamani hivyo kwanini alitaka kufanya cri kwa mkewe? c angemueleza tu lengo lako kuliko aje aickie baada ya tukio......cna msaada! na hizo tamaa zenu mtabambikiwa sana tu.
 
Yani ni sawa na ule msemo kuwa muuzaji(machinga) kauza cheni ya gold bandia na mnunuaji katoa pesa bandia naye.Hapo imekula kwao wote wawili.
 
...jamaa kaamua kudai mahari yake, mke basi!
inasikitisha lakini ndio hivyo tena, heri ya nusu shari...🙁

...na nyie Bro's wangu mnaobonda humu mmepima?
ndoa zimeingiliwa, msijitutumue vifua mbele kumbe DNA mgogoro...
msijidanganye na oooh, "...ana mwanya kama wangu, charangi kama shangazi yake...!"

mwenzenu nishajicheki na wanangu!
 
Ha, ha, haaaaa.
Mbu. safi sana .sema nao
 
...aaah, si unajua tena...ruksa kuoa wanne, na kumuarifu mke ni sunna tu!

...hata asipomchukua yeye, Viza keshapata! ...Qatar airways ticket bei chee tu...

Sawa, aende na nauli yake.
 
...jamaa kaamua kudai mahari yake, mke basi!
inasikitisha lakini ndio hivyo tena, heri ya nusu shari...🙁

...na nyie Bro's wangu mnaobonda humu mmepima?
ndoa zimeingiliwa, msijitutumue vifua mbele kumbe DNA mgogoro...
msijidanganye na oooh, "...ana mwanya kama wangu, charangi kama shangazi yake...!"

mwenzenu nishajicheki na wanangu!

ahahahah ati mahari kadai? mi nimesema dawa yake hiyo..

eh nawewe umepima DNA ulidiscuss na my your wife ama ulifanya kiujannja tu? pili its easy kwa huko majuu hapa third world jamani DNA sio ya kila mtu.
 
...jamaa kaamua kudai mahari yake, mke basi!
inasikitisha lakini ndio hivyo tena, heri ya nusu shari...🙁

...na nyie Bro's wangu mnaobonda humu mmepima?
ndoa zimeingiliwa, msijitutumue vifua mbele kumbe DNA mgogoro...
msijidanganye noooh, "...ana mwanya kama wangu, charangi kama shangazi yake...!"

mwenzenu nishajicheki na wanangu!

Hivi Mbu hadi uliamua kwenda kucheki DNA ya watoto wako hukumuamini mkeo?

Je na watoto hawajafanana na wewe kiungo chochote...........mfano pua, macho, mdomo, masikio, kichwa na vidole!!
 
...jamaa kaamua kudai mahari yake, mke basi!
inasikitisha lakini ndio hivyo tena, heri ya nusu shari...🙁

...na nyie Bro's wangu mnaobonda humu mmepima?
ndoa zimeingiliwa, msijitutumue vifua mbele kumbe DNA mgogoro...
msijidanganye na oooh, "...ana mwanya kama wangu, charangi kama shangazi yake...!"

mwenzenu nishajicheki na wanangu!

Mbu unanipaga raha sana....hivi mtu anaanzaje kukwambia tukacheki DNA ni kwamba ameshakuwa na wac sio wanae au ni kipi hasa, hawa wangu wamefanana na baba yao kivivyo then cku aniambie mambo hayo looo....au unaenda kimya?
 
Back
Top Bottom