Akilimali: Kama kuna mtu anataka kuiacha familia yake aje avamie nyumbani kwangu

Akilimali: Kama kuna mtu anataka kuiacha familia yake aje avamie nyumbani kwangu

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi!

Kama mjuavyo Mzee Akilimali ndiye anaye jua yanga ilipo.
Baada ya baraza la wazee wa Yanga kumsimamisha mzee Akilimali uanachama huyu mzee aliona akae kimya bila kusema chochote kile.

Lakini walizuka baadhi ya wanachama wa Yanga hasa vijana wakitaka na kupendekeza mkutano mkuu umvue uanachama wa Yanga kabisa mzee Akilimali .. Bado mzee huyu alinyamaza kimya..

Baada ya mechi ya dhidi ya Azam FC walisikika vijana wakipanga kwenye kumvamia mzee Akilimali nyumbani kwake ili kumfanyia vurugu wakiamini yeye ndio sababu za mvurugano ndani ya Yanga.

Baada taatifa hizo kumfikia mzee Akilimali kupitia E-FM alitoa onyo kali kwa yeyote au kikundi chochote kitakacho gusa kwake na kwenda kufanya vurugu..
Mzee Akilimali alisema

Kama kuna mtu anataka kuicha familia yake aje kufanya vurugu nyumbani kwangu, pia aliongeza kuwa kama kuna mtu anataka kuhama mji bila kupenda basi aje kunifanyia vurugu...

Hata hivyo baada ya onyo hilo kwa mashabiki wa Yanga hakuna aliyegusa kwa mzee wa mjini Akilimali.

Mzee Akilimali alipopigiwa simu kuulizwa alise hajaona mtu yetote kwake ana aliogeza kwa kusema yeye ana Mungu na akasema tena kama kuongea vile kulimuudhi Manji alishaomba radhi na amesema Manji mwenyewe wakishasameheana na Manji hajajiuzulu uenyekiti wa Yanga..

Alipoulizwa kuwa jana hakulala kwake alicheka akasema anayesema si kulala kwangu alifika?

Ushauri.
Wanachama wa Yanga mnapoteza muda kupambana na huyu mzee hamtomuweza yeye ndio anajua Yanga ilipo fichwa.!

Karibuni wana jamvi.
 
Huyu mzee sijui anatumia uchawi wa wapi.....maana kawaroga wanachama wa Yanga wote.....mpaka Manji mwenyewe kampa limbwata......
Wamekuwa kama mazezeta tu mbele ya huyu mzee.....ngoja tungoje mkutano mkuu kama wana ubavu wa kumvua huo uanachama......
 
Hahahaha amesema yupo kwake ana wasubiri...
 
Mambo haya ndiyo yalinifanya niache kuishabikia Yanga pamoja na hizi timu zetu za 'kiswahili'. Kwa kauli hizi zinanisaidia kuendelea kuamini kuwa maamuzi yangu ya kuachana na upenzi wa hizi timu yalikuwa ni sahihi!
 
Huyu mzee ni jabari huwa hachezewi ovyo na uanachama hawawezi kumvua anaetaka,kumvua aanze yeye asiwasingizie wenzie wakatangulia familia zao zipate shida bure..
Hahahahaha Kasema kabisa ambaye hataki kubaki na familia yake akamfate kwake afanye vurugu...

Kasema walisha sameheana na Manji sasa wengine wanaleta choko choko..
 
Mambo haya ndiyo yalinifanya niache kuishabikia Yanga pamoja na hizi timu zetu za 'kiswahili'. Kwa kauli hizi zinanisaidia kuendelea kuamini kuwa maamuzi yangu ya kuachana na upenzi wa hizi timu yalikuwa ni sahihi!
Hahahahahaha mkuu kwani ulipanga kwenda kumfata mzea Akilimali kwake?
 
Ovyo mujarabu kabisa.. Na huenda huyu mzee kuna kitu anategemea, haiwezekani kauli zake kidogo tu.. si manji si wanachama pamoja na mashabiki wanataharuki
 
Ovyo mujarabu kabisa.. Na huenda huyu mzee kuna kitu anategemea, haiwezekani kauli zake kidogo tu.. si manji si wanachama pamoja na mashabiki wanataharuki
Huyu ndiye anajua Yanga ilipo...
 
Sioni tofauti kati ya siasa za kibongo na ligi zetu za mpira. Ni vituko kwenda mbele huku maendeleo hayaonekani kwa pande zote mbili.
 
Sioni tofauti kati ya siasa za kibongo na ligi zetu za mpira. Ni vituko kwenda mbele huku maendeleo hayaonekani kwa pande zote mbili.
Hahahahaha Mzee kasema wajaribu..
 
Hahahahaha Kasema kabisa ambaye hataki kubaki na familia yake akamfate kwake afanye vurugu...

Kasema walisha sameheana na Manji sasa
wengine wanaleta choko choko..
Vijana wanatafuta ubaya mzee wa watu bora wamuache tu,maana kuna watu wanajifanya wanaijua yanga kuliko Mzee Akilimali wakati ni wa juzi tu.
 
Kama kuna kitu miye nadharau hapa Tz ni mwanamichezo. Hata mcheza bao, karata na draft. Namdharau. Badala ya mazoezi heavy na akili nyingi watu wanahama nyumbani wanahamia Mlingotini na Pemba ati kusindikwa. Sijui wamekuwa nyanya au nyama!! Jamani, pigeni hadithi na kina Kanu na Drogba. Wawaeleze siri ya mafanikio yao.
Mnatishwa na "vijini" vya Akilimali. Mnaacha kutafuta wachezaji wenye kujituma wakiwa uanjani mnawategemea watumainia hirizi. Niliachaga kucheza mpira tangu nikiwa chuoni kwa sababu tu kocha aliniletea hirizi ati niivae. Kwa sababu nilikuwa nampenda sana kocha nikaona nisimuudhi. Kuivaa tu, hata kabla ya half time, mguu ukavunjwa mara 2. Nikajuta kuivaa hirizi yake.
Tujiulize. huko Pemba ka kuna ndumba ya mpira, kumetoka timu ngapi bora?? Huko mlingotini Bwagamoyo, timu yao ya wilaya ni ipi?? Acheni uzuzu, piga zoezi heavy na soma tricks za mchezo, vaa moyo wa kujituma ukijua kuwa michezo ni kazi na ajira ka vile Accounts au IT. Kalaghabao na ubozi wenyu wanamichezo wenzangu. Msinichukie ni mawazo yangu tu wala sijamtukana mtu.
 
Back
Top Bottom