Akilimali: Kama kuna mtu anataka kuiacha familia yake aje avamie nyumbani kwangu

Akilimali: Kama kuna mtu anataka kuiacha familia yake aje avamie nyumbani kwangu

Wewe jana ulikwenda kwake?
Aende hajitaki haya ni maneno ya kwenye maandishi tu, hebu jiulize hao anaowasema walienda kwa mzee Akili, waliingia mpaka ndani kumtafuta au waliulizia nje. Kama hawakuingia ndani kumtafuta walijuaje hayupo.
 
Kama kuna kitu miye nadharau hapa Tz ni mwanamichezo. Hata mcheza bao, karata na draft. Namdharau. Badala ya mazoezi heavy na akili nyingi watu wanahama nyumbani wanahamia Mlingotini na Pemba ati kusindikwa. Sijui wamekuwa nyanya au nyama!! Jamani, pigeni hadithi na kina Kanu na Drogba. Wawaeleze siri ya mafanikio yao.
Mnatishwa na "vijini" vya Akilimali. Mnaacha kutafuta wachezaji wenye kujituma wakiwa uanjani mnawategemea watumainia hirizi. Niliachaga kucheza mpira tangu nikiwa chuoni kwa sababu tu kocha aliniletea hirizi ati niivae. Kwa sababu nilikuwa nampenda sana kocha nikaona nisimuudhi. Kuivaa tu, hata kabla ya half time, mguu ukavunjwa mara 2. Nikajuta kuivaa hirizi yake.
Tujiulize. huko Pemba ka kuna ndumba ya mpira, kumetoka timu ngapi bora?? Huko mlingotini Bwagamoyo, timu yao ya wilaya ni ipi?? Acheni uzuzu, piga zoezi heavy na soma tricks za mchezo, vaa moyo wa kujituma ukijua kuwa michezo ni kazi na ajira ka vile Accounts au IT. Kalaghabao na ubozi wenyu wanamichezo wenzangu. Msinichukie ni mawazo yangu tu wala sijamtukana mtu.
hayo ndiyo mawazo ya kiume good
 


Hizi ni mikwara tu! Kwanini nasema hivyo?

Siku moja kabla hajahojiwa na kituo cha Efm radio baadhi ya wanachama wa Yanga SC walimfuata kwake maeneo ya tandale majira ya saa 11 Jioni, baada ya kupata taarifa kuwa Mashabiki wa Yanga wamemfuata kwake basi ikabidi aongee na uongozi wa msikiti mkuu wa Tandale ili japo apate kulala mahala pale kwa siku.

Asubuhi baada ya kujulishwa kuwa wale vijana wa Yanga waliondoka ndipo akaamua kurudi kwake.

Baada ya habari hizi kuenea kote, ndipo e fm aalimtafuta na kuanza kumfanyia mahojiano, ambapo alianza kwa kutoa vitisho kwa yeyote atakaye kuja kwake!

SWALI: Kama anajiamini na uchawi wake kwanini hakurudi kwake usiku ule, mpaka akalala msikitini?
Maneno mengi ya nini mheshimiwa amesema mfuate na umuulize.
 
Nan anataka kugeuzwa kuwa shoga? Thubutuuuu! Nenden nyie mnaojiona kuwa ni wababe
 
Nilikuwa najenga mapenzi kwa timu kama Toto Afrika lakini nikaja kugundua eti nao wanajiita tawi la hawa manyang'au wa mpira. Najaribu kwa Lipuli sasa maana upenzi wa game ninao lakini tatizo ni jinsi linavyoendeshwa. Ndio maana juzi nilikuwa maangali michezo ya majeshi Kigali (Soccer TZ-Kenya) na ilinivutia zaidi kuliko kuangalia hizi so called timu!
lipuli tawi la simba
 
lipuli tawi la simba
Nasoma gazeti la Habari leo eti limetoa ratiba ya ligi ya EPL kwa leo, bora mwananchi wametoa ratiba ya ligi yetu.
Alafu kwa mentality kama hizi utegemee eti mpira wetu utaendelea siku moja!
 
Aisee hapo hatii mtu mguu chezea Akili Mali.
 
Wasalaam wana jamvi!

Kama mjuavyo Mzee Akilimali ndiye anaye jua yanga ilipo.
Baada ya baraza la wazee wa Yanga kumsimamisha mzee Akilimali uanachama huyu mzee aliona akae kimya bila kusema chochote kile.

Lakini walizuka baadhi ya wanachama wa Yanga hasa vijana wakitaka na kupendekeza mkutano mkuu umvue uanachama wa Yanga kabisa mzee Akilimali .. Bado mzee huyu alinyamaza kimya..

Baada ya mechi ya dhidi ya Azam FC walisikika vijana wakipanga kwenye kumvamia mzee Akilimali nyumbani kwake ili kumfanyia vurugu wakiamini yeye ndio sababu za mvurugano ndani ya Yanga.

Baada taatifa hizo kumfikia mzee Akilimali kupitia E-FM alitoa onyo kali kwa yeyote au kikundi chochote kitakacho gusa kwake na kwenda kufanya vurugu..
Mzee Akilimali alisema

Kama kuna mtu anataka kuicha familia yake aje kufanya vurugu nyumbani kwangu, pia aliongeza kuwa kama kuna mtu anataka kuhama mji bila kupenda basi aje kunifanyia vurugu...

Hata hivyo baada ya onyo hilo kwa mashabiki wa Yanga hakuna aliyegusa kwa mzee wa mjini Akilimali.

Mzee Akilimali alipopigiwa simu kuulizwa alise hajaona mtu yetote kwake ana aliogeza kwa kusema yeye ana Mungu na akasema tena kama kuongea vile kulimuudhi Manji alishaomba radhi na amesema Manji mwenyewe wakishasameheana na Manji hajajiuzulu uenyekiti wa Yanga..

Alipoulizwa kuwa jana hakulala kwake alicheka akasema anayesema si kulala kwangu alifika?

Ushauri.
Wanachama wa Yanga mnapoteza muda kupambana na huyu mzee hamtomuweza yeye ndio anajua Yanga ilipo fichwa.!

Karibuni wana jamvi.
 
Back
Top Bottom