Al-Ahly inamaanisha "Taifa", hivyo unaweza kuita 'Club ya kitaifa' Hizi hapa Timu za kiarabu na maana zake

Al-Ahly inamaanisha "Taifa", hivyo unaweza kuita 'Club ya kitaifa' Hizi hapa Timu za kiarabu na maana zake

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
(1) Jina la 'Al-Ahly SC'
Jina lilipendekezwa na Amin Samy Amin, ambaye alipendekeza kuwa jina hilo ni sawa na neno "taifa" katika Kiarabu cha Misri. Lengo la jina ni kuwahudumia wanafunzi na wahitimu wa shule ambao walikuwa mhimili mkuu wa mapinduzi dhidi ya uvamizi wa Uingereza nchini Misri.

1711738832029.png

(2) Al-Hilal' Saudi Club'
Maana halisi ya jina Al-hilal ni 'Mwezi mpevu' Jina hilo walipewa na Mfalme Saud. Alibadilisha jina lao na kuwaita Al-hilal baada ya kuhudhuria mashindano ambayo yalishindaniwa kati ya Klabu ya Olimpiki, Vilabu vya Al Nassr, Al Riyadh na Al-Kawkab.

1711738768696.png

(3) Al-Ahli Saudi Club'
Al-Ahli, ni klabu ya soka ya Saudia yenye makao yake mjini Jeddah. Al-Ahly ni kama ile ya Misri maana yeke ni 'Club ya Taifa' kwa maana neno Al-Ahli (Taifa au Familia).

1711738966306.png

(4) Zamalek SC
Kufuatia mapinduzi ya Misri ya 1952 na kupinduliwa kwa Mfalme Farouk, klabu hiyo iliitwa Zamalek Sporting Club (Zamalek SC) baada ya eneo ambalo klabu hiyo ilikuwa. Zamalek ni kisiwa katika Mto Nile. Ni jina la Kata ndani ya Wilaya ya Magharibi katika Eneo la Magharibi la Cairo, Misri. Neno 'Zamalek' ni kibanda kidogo cha mbao kilichojengwa kwenye kingo za mito ndio huitwa Zamalek.
1711739086610.png

(5) Wydad AC
Wydad ni neno la Kiarabu linalomaanisha "upendo", "mapenzi ya dhati.", wakati wa mikutano yao ya mara kwa mara huko Moroco ambayo ilisababisha kuundwa kwa klabu, mmoja wa wanachama waanzilishi alipendekeza jina hilo.

1711739184569.png

(6) Al-merrikh sporting club
Neno Al-merrikh humaanisha "kusugua", "kuvuja utomvu' (hasa mafuta yanayoweza kuwaka)" "kusugua pamoja matawi yanayoweza kuwaka"; inayotokana na rangi nyekundu ya sayari kuhusishwa na moto. Al-merrikh ni sayari ya nne iliyo mbali zaidi na jua katika mfumo wa jua. Ni sayari nje ya Dunia na imeainishwa kama sayari yenye miamba, kutoka kundi la sayari za dunia, sayari yenye tabia ya kusugua na kuwaka.

1711739231600.png

(7) Al-Nassr Saudi Club
Al Nassr ni neno la Kiarabu la "ushindi", vilabu vyenye jina moja vinapatikana Oman, Kuwait, Bahrain, UAE, na Libya lakini klabu ya Saudi Arabia ilikuwa ya kwanza kuchukua jina hilo. Nembo ya klabu inawakilisha ramani ya Uarabuni yenye rangi ya njano na bluu.

1711739308097.png

(8) Raja Club Athletic,
Inajulikana pia kama Raja Casablanca, ni klabu ya kandanda yenye makao yake mjini Casablanca, Morocco, ambayo inashiriki ligi kuu ya soka ya Morocco. 'Raja' imetokana na 'ar-Raja' 'ar-Riyady' inayomaanisha 'tumaini' kwa Kiarabu.

1711742618835.png
 
Back
Top Bottom