Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.

Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini.

Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni.

Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.

Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430
Hii ni kwa mujibu wa kile kitabu cha hadithi sio?
 
Acha ujinga na dini yako yamashetani na upuuzi unakili maisha baada ya kufa siri anaijua MUNGU we unaelezea umeyatoa wapi je we Uncel wa Sir GOD ama [emoji23] yaan ujinga wa waarabu unatuletea sis [emoji23] mavi yakiwa na muumini tumboni si haramu anaingia nayo msikitini akifa mavi ni haramu hayafai kuingia nayo kaburini yakamuliwe huo si ujinga
 
Hakika yote aliyoyasema allah ni ya kweli na yapo wanaobisha waache wabishe but nawasihi nyie mnaokanusha Rudini kwa allah kabla aujawafikieni msiba mzito . kuna adithi inaeleza kuna mtu alimuendea mtume muhamad s.a.w akamuuliza ewe mtume wa mungu je lipi ni jambo gumu apa duniani, mtume muhamad s.a.w akamjibu jambo gumu ni kaburi na gumu zaidi ni pale unapoliendea bila ya maandalizi ..Adhabu za kaburi zipo atakayebisha ata prove mwenyewe siku atakayokufa na kuzikwa.
 
Back
Top Bottom