Al Hilal anapoenda kutukung'uta mechi ijayo, naomba mtakapomtimua Gamondi timueni na wachezaji wafuatao

Umeongea maoni yako ila hapo kwa Chadrack Boka na Khalid Aucho nadhani umekosea, Bila shaka umeona game ya leo bila hao watu + Clement Mzize game inapoa sana. Angalau ungesema Dube + Bacca watafutiwe mbadala. Kocha wa viungo na fitness naye anapwaya sana, wachezaji hawako fit kabisa, Kabla ya hii mechi, Manager na benchi lote la ufundi ilipaswa kupata mechi moja ya kirafiki ili kocha mpya awatambue wachezaji na wachezaji wawe fit, Jambo ambalo halikufanyika. Anahitajika striker mbadala wa Dube, na Namba 9 hatari kama Mayele. Kingine ni ari ya uchezaji ipo chini sana,ambayo inaweza kubadilishwa wakija wachezaji wapya dirisha dogo. Hayo tu, YANGA BINGWA.
 
Umeweka hiyo list yote ya wachezaji Wa kigeni, Je unazijua Sheria za TFF kuhusu namba ya wachezaji Wa kigeni wanapaswa kuwa kwenye team husika?

2. Je hiyo list uliyoweka na Ukasisitizia na wawe na uzoefu Wa kutosha na Ubora WA Kiwango cha Juu, Je Umefikia kuhusu gharama zao za usajili na mshahara Yao kuwalipa???

Yangu ni Hayo Tu.
"Daima mbele, Nyuma mwiko"
 
Kwani ubora hua unaangalia gharama au kuscout kipaji..? Kuna wachezaji wamekuja hawana majina na kwa bei chee tu lakini ndo wanafanya mabalaa...
Mayele, maxi, yao, Tadeo Lwanga, Kipre Jr ni mfano wao
 
Acha wenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…